https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZ0dOVOoNtujZkfP2CxOCV12D3lGJp26bqxhtiQraBhQB6GFtugg8dRX3NOuzDGQu9bEr4PM0Xnf6MISBXtSrS-UncgGOTNF86fIh9Sq8jZqgQWxb7TMHBta2WJUlqrE7SQyv9WRTf54M/s1600/Untitled.png

LICHA ya kuwa na warembo wa kutosha, Nollywood, inaelezwa kuwa ni eneo lisilokuwa na wanawake wengi walio kwenye ndoa.
Wanawake wengi waliomo katika eneo hili ni ama hawajaolewa au wametalikiwa. Pamoja na hao, pia kuna kundi jingine ambalo ni la wanawake waliokubali kuolewa uke wenza wakiwa wake wa pili kwenye ndoa zao.
Mtandao wa Vanguard umefanya mahojiano na waigizaji wa Nollyhttps://www.blogger.com/blogger.g?blogID=3837554060892175300&pli=1#editor/target=post;postID=60101471186193387wood walio katika ndoa za uke wenza wengi wao wakiwa ni wake wa pili na kutaka kujua ni kwanini hasa waliamua kuingia kwenye uhusiano huo.
Wengi wao walioingia kwenye aina hiyo ya ndoa wameonja joto ya jiwe kwani siku zote maisha yao yamekuwa katika mapambano na wenye waume zao. Pia wapo waliokuwa na bahati wanaoishi maisha ya raha mustarehe.
Wafuatao ni miongoni wa wanawake walioolewa na waume wa wenzao.
Caroline Ekanem-Danjuma
Stori ya mwigizaji huyu mwenye mvuto kutoka Nollywoodv ipo wazi. Alikuwa miongoni mwa mastaa waliokuwa wakivutia zaidi waonekanapo kwenye runinga. Ni mke wa pili wa bilionea Musa Danjuma.
Baada ya kuingia kwenye ndoa hiyo, mwigizaji huyo aliyeachana na uigizaji ili kuijenga ndoa yake, amekuwa akiishi maisha ya raha zaidi.
Hata hivyo wajuzi wa mambo wamekuwa na shaka juu ya ndoa ya msanii huyu hasa pale alipoandika kwenye ukurasa wake wa Facebook akisema “Chaguo la pili si kazi rahisi”.
Liz Dasilva
Pamoja na kuwa hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa mwigizaji huyo chotara wa Togo/Nigeria ameolewa na baba wa mtoto wake aliyezaliwa miezi michache iliyopita, lakini kilicho wazi ni kuwa mwigizaji huyo amesilimu na kuwa Mwislamu akifuata dini ya mumewe, Alhaji Olaoye. Inasemekana kuwa Liz ni miongoni mwa wanawake wengi walioolewa na Alhaji Olaoye.
Mercy Aigbe 
Naye ni miongoni mwa mastaa wa Nollywood waliokomaa na waume za watu. Tofauti na wenzake, Mercy Aigbe, ameingia kwenye ndoa ya mwigizaji mwenzake, Lanre Gentry, na hivyo kuwa mke halali wa Bimbo Akinsanya.
Ini Edo
Staa huyo aliolewa na mfanyabiashara, Philip Ehiagwina,
mwaka 2009. Jamaa huyo maskani yake ni Texas, Marekani.
Tangu alipoingia kwenye uhusiano huo, ndoa yao imekuwa kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari kila uchao. Si kwa kuwa habari za Edo zinawavutia sana wasomaji, bali kwa sababu Edo amepora mume wa mtu.
Ehiagwina ni mume halali wa mwigizaji na mwanamitindo, Ruth Okoro. Hata hivyo, Ruth aliamua kuondoka na kumwachia Ini Edo mume.
Bose Arowosegbe
Kama ulikuwa ukijiuliza kwa nini waigizaji wa Nollywood wanapenda kuolewa na waume za watu, wala huna haja ya kuendelea kujiuliza. Ni kwa sababu mwigizaji, Bose Arowosegbe, amefunguka na kuweka hadharani sababu inayowasababisha wafanye hivyo.
Anasema wanaume wasiowahi kuoa huwa na utoto mwingi pia wengi wao ni maskini. Kwa hali hiyo inakuwa ni vigumu kuweza kwenda sawa na hadhi ya wanawake waigizaji kama wao.
“Nimeamua kuolewa na mume wa mtu kwa kuwa ana uwezo wa kuwa na mimi kwa kila hali,” anasema.
Mercy Johnson
Mwigizaji mwenye mafanikio makubwa Nollywood. Anajulikana kwa kazi zake nzuri anazofanya. Upande wa pili wa mwigizaji huyo ni tofauti kabisa. Ameolewa na mume wa mtu tena mwenye watoto watatu; wawili wa kiume na mmoja wa kike.
Anayatamani haya
Japokuwa Lulu amepata mchumba, anasema katika maisha yake alikuwa akitamani kuyapata mambo yafuatayo ili awe amekamilika kama mwanamke.
“Nina mchumba lakini katika maisha yangu nilikuwa natamani sana kupata mwanamume mwelewa, atakayenielewa, atakayeweza kutunza familia na si pesa zitunze familia, nahitaji mwanamume anayejituma na kujali familia yake.
“Kikubwa zaidi nilikuwa natamani kuwa na mwanamume atakayeielewa kazi yangu na kila kitu changu. Nashukuru Mungu kwani yule niliyekuwa namwomba nimempata lakini itategemea siku zijazo hasa pale kila kitu kitakapokamilika. Nasikitika kwamba siwezi kumweka wazi kwa sasa, lakini ipo siku nitahitaji watu wamjue,” anasema.
Kuhusu msimamo wake kwa mwanamuziki mwenye umri mdogo kutoka nchini Marekani Justine Bieber Lulu anasema;
“Nampenda Justine Bieber japokuwa nimepata mchumba, mimi ni shabiki wake mkubwa natamani kuolewa naye, Lulu ni mtu mmoja wa ajabu sana na hafanani na vile watu wanavyomdhania, ila ipo siku nitahitaji watu wamjue zaidi huyu binti ni nani na ni mtu wa aina gani,” anasema.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment