MTOTO WA MIAKA 4 DEVOTHA GERLAD ALIYEKATWA MAPANGA NA BABA YAKE,HAPA AKIWA HOSPITALI AKIPATIWA MATIBABU.
WANANCHI WAKIWA NJE YA HOSPITALI YA WILAYA WAKIWA NA SHAUKU YA KUMUONA MTUHUMIWA.
KINA MAMA WALIOGUSWA NA TUKIO WAKIWA NJE YA HOSPITALI KUMUONA MTOTO HUYO.
AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI
AFANDE AKIWA HOI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALINI..
MADAKTARI WAKIJITAHIDI KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO.
MADAKTARI WAKIJITAHIDI KUMPATIA MTOTO DEVOTA MATIBABU ILI KUMNUSURU NA KIFO..
AFANDE BWIRE AKIWA HOI WODINI HUKU AKIWA AMEFUNGWA PINGU.
JITIHADA ZA KUOKOA MAISHA YA MTOTO
INASIKITISHA SANA JAMANI
MAJUKUMU YA KUOKOA MAISHA YA MTOTO HUYO
AFANDE BWIRE AKIWA NA PINGU ZAKE WODINI
MUNGU AMPE AHUENI MTOTO HUYU.
MKAZI mmoja wa kitongoji cha Sango kata ya Nyasubi wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Samson Bwire (54), anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kumcharanga kwa mapanga mtoto wake Devotha Gerald (4) kwa sababu za wivu wa kimapenzi. Tukio hilo limetokea leo jioni nyumbani kwa Bwire baada ya kuanza kugombana na mke wake Happiness (28) Elias huku akiwa amelewa pombe ambapo, mkewe alikimbia kitu kilichosababisha kumgeukia mtoto Devotha na kuanza kumkata mapanga kichwani. Kwa mujibu wa majirani, kelele zilisikika kutoka kwenye mji huo na kwamba walipoenda walimkuta Bwire akizichoma moto nguo za mke wake, na alipowaona aliingia ndani na kuanza kumkata kw panga mtoto huyo huku akiwa amefunga mlango.
Imefafanuliwa kuwa, baada ya kusikia kelele za mtoto, majirani walianza kuvunja milango huku wakiomba msaada kituo cha Polisi na baada ya Polisi kufika walifanikiwa kumnusuru mtoto akiwa amejeruhiwa vibaya sehemu za kichwani. Majirani kwa hasira walianza kumpiga Bwire ambaye ni askari polisi mstaafu wa cheo cha koplo kwa nia ya kumwua, hali ambayo imelipa jeshi la Polisi kazi ya ziada kumnusuru na kumpakia kwenye gari kwenda kituoni.
Hata hivyo Wakati gari la Polisi likiwa katika mwendo wa kasi eneo la soko la Mkulima, Bwire ameruka kutoka kwenye gari na kuangukia kwenye Lami kitendo kilichomsababishia majeraha makubwa sehemu za usoni.
Mtoto Devotha na baba yake Bwire wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa matibabu huku Bwire akiwa Chini ya Ulinzi mkali wa polisi.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment