| |||
Labda wadada wenzangu mlio wakubwa na wazoefu mwaweza kunisaidia juu ya hili. Hivi umeshatoka na mtu ambaye ameoa, amekuzidi umri lakini he is a total package!??? Yaani, he is so good na nikijaribu kutoka na mkaka wa umri wangu, anazingua, na hajui (hawajui) kabisa 'vitu vingi', Hii imekaaje, yaani inachanganya sana!!! niko kwenye late twenties, well educated/financially stable and independent, lakini kwa hapa nimekwama, nadhani nahitaji shule tofauti ya masuala haya.BF wangu aliyepita kabla huyu bwana, alikuwa 4years older than me, nilimtosa maana alikuwa kicheche mno, na nilivumilia madudu yake mengi,nikjipa matumaini kwamba sisi bado tu vijana na umri unaturuhusu, tuta cope kadiri muda unavyoenda - lkn nikashindwa! huko nyuma my first love, aliendaga kuoa bila kuniambia akidai kwamba alilazimishwa na familia - nikachoka, mwisho nikaamua kubwanga manyanga kuhusu masuala ya wanaume na ku focus na shule na career -na kwa kweli I am doing very well hadi nilipokutana na huyu wa sasa. Nilikuwa nimekaa muda mrefu bila 'kuwa na mwanaume'. nnilivutiwa naye hasa personality na mitazamo yake kimaisha, na ilikuwa kama utani na wala sikuwa na mpango naye sana, nilikuwa 'napita tu' he made it very clear kwamba ameoa na asingependa kwa namna yoyote ile ku compromise ndoa yake. Yaliyobaki ni historia, nimejaribu mara kadhaa kudate vijana wenzangu lakini kwakweli walio wengi 'hamna kitu' yaani I feel nothing for them, hawajui 'kuongea' hawajui jinsi ya 'kumtreat mwanamke inavyotakiwa' wana haraka kwa kila kitu, I will pay and do any thing for this guy. Nimejaribu kumwomba nizae naye and I can take care of the baby, on my own lakini kakataa, akaniambia kwamba: " You are young, smart and beautiful with a bright future, you deserve something better than me I am here to help you achieve that, na kila mara ananimaliza kwa kusema kwamba ' If you want I will be out of your way whenever you are ready to move on"! Jamani nifanyeje maana umri nao ndio huo unasogea, maana nilipanga nitakapofika miaka 30 angalau tayari niwe na ka baby kangu mwenyewe, lakini wanaume wako wapi?????? I am the one who needs him so badly, and he has been there for me all this time, please help! |
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment