MWIGIZAJI mkongwe Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ amefunguka kuwa levo aliyofikia hivi sasa ni ya kuweza kusimama mwenyewe na anaweza kusimamia filamu pasipo mkurugenzi mwenzake wa Kampuni ya RJ Company, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Akizungumza na paparazi wetu, Johari alisema yeye na Ray wamejiwekea mikakati yakinifu katika majukumu ya kazi ndiyo maana anaweza kuigiza filamu peke yake na Ray vilevile.
“Mimi na Ray hatutegemeani, mfano sasa hivi mimi naandaa filamu ya Bad Lucky ambayo Ray hakushiriki kwa kitu chochote,” alisema Johari.
Vincent Kigosi ‘Ray’.
Source: GPL
TUPE MAONI YAKO HAPA:

0 comments:
Post a Comment