WATOTO wenye asili ya Kiarabu wamezua tafrani ya aina yake baada ya kumkomalia mwigizaji Jacqueline Wolper apige nao picha.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo ya Magomeni-Mapipa, Dar kwenye shughuli ya arobaini ya mtoto wa mwigizaji Halima Yahya ‘Davina’ ambapo uvumilivu uliwashinda walipomuona staa huyo, wakaanza kumsumbua mama yao awaombee ili wapige naye picha.
Kutokana na umri wao kuwa mdogo, mama yao alishangazwa na kitendo cha wanaye hao kumjua mwigizaji huyo ingawa hakuwa na jinsi, ilibidi amuombe Wolper apige picha na wanaye.
Wakati zoezi la kupiga picha likiendelea, watoto hao walionekana kumshangaa Wolper huku wakimshika sehemu mbalimbali za mwili wake.
LIKE PAGE YETU HAPA ILI UWEZE KUPATA HABARI ZETU KUPITIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK KILA SIKU.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment