Obama akicheka na Mke wa Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon (hayupo pichani), kushoto kwake ni Mkewe mama Michelle Obama.
 Hapa wakiteta jambo Obama na Mke wa Cameroon.
 
 Hapa wakioneshana kijarida cha kumbukumbu cha hayati Mzee Madiba Mandela katika viwanja vya FNB Soweto Jijini Johannesberg Afrika ya kusini.
 
 Viongozi:Tony Abbott, John Key and David Cameron, mawaziri wakuu wa Australia , New Zealand na Uingereza wakiwa katika maombolezo hayo ya kifo cha shujaa wa Afrika na Dunia Mzee Mandela.
 
 Obama akipunga Mkono kuwasalimu umati wa watu katika viwanja hivyo vya FNB Soweto Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini. 
 
Obama Rais wa Marekani akitoa salamu za pole kwa mama mjane wa Mzee Mandela, Gracia Machel katika viwanja vya FNB Soweto Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini jana.
 
Obama akimbusu Mjane wa Mzee Mandela mama Gracia Machell Mandela.
 Obama akitoa hotuba fupi katika hafla hiyo ya maombolezo ya msiba huo mzito uliokutanisha Marais zaidi ya 90 katika uwanja wa FNB Soweto Jijini Johannesburg Afrika ya Kusini hapo jana.
 Si kwamba kuna mechi ya mpira lah hasha!ni umati mkubwa wa watu toka nchi mbalimbali pamoja na marais 100 wa dunia, katika maombolezo ya pamoja kufuatia kifo cha Mzee Madiba Mandela.
 Obama akisalimiana na Raul Castro ambaye ni kaka wa Rais wa Zamani wa Cuba Fidel Castro, kitendo kinachochukuliwa kuwa ni cha kihistoria na kuwa msiba huo umeleta historia kwa wawili hao.
 
Hapa tena Rais Obama akisalimiana kwa ukaribu zaidi na kaka huyo wa Rais wa Zamani wa Cuba Fidel Castro.
 
 Barrack Obama akicheka na Mke wa waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon(hayupo pichani) kushoto kwake ni mkewe Michelle.
 
Familia ya Mzee Mandela wakiwa katika kundi la pamoja, wazazi, wajukuu na vitukuu pamoja na ndugu na jamaa wa karibu wa familia hiyo.
 
Obama Rais wa Marekani akisalimia na Rais wa Afrika ya Kusini Jackob Zuma , kushoto ni Ban Ki-Moon Katibu Mkuu Umoja wa Matifa yaani UN
 
Winnie Mandela mtalaka wa hayati Mzee Mandela katika majonzi makubwa juu ya kifo cha shujaa huyo.
 
Mjane mama Gracia Machel Mandela akiwa katika hali ya huzuni juu ya msiba mkubwa wa mzee Madiba.
 
Obama Rais wa Marekani akisalimiana wa raia wa Afrika ya kusini uwanja wa FNB Soweto.
 Bill Clinton Rais Mstaafu wa Marekani pamoja na familia yake Mke mama Hillary pamoja na mtoto wao Chelsea.
 
Barrack Obama Rais wa Marekani na Mkewe Michell kushoto kwake wakitazama kijarida kinachomuhusu hayati Mzee Mandela.
 
Hii ni familia kubwa ya marehemu Mzee Mandela, pamoja na ndugu na jamaa wa karibu.
 
Hivi ndivyo inavyoonekana umati wa watu ukiwa umefurika, huku wengine wakijaribu kukwepa mvua iliyokuwa ikinyesha.
 
Winnie Mandela na Mama Machel Mandela mjane wa Mzee Mandela wakibusiana ishara ya kupeana faraja,wawili hao inasemekana wanaishi kama mtu na dada yake.
 Winnie Mandela Matalaka wa Hyati Mzee Mandela akiwa katika hali ya majonzi juu ya kifo cha shujaa huyo. 
 Huu ni umati wa watu katika uwanja huo wa FNB Soweto wakiwa katika maombolezo ya kifo cha Mandela, huku wakiwa wamejifunika miamvuli kujikinga mvua iliyokuwa ikinyesha.
 
Barrack Obama Rais wa Marekani akimuonesha mkewe Michelle kijarida cha kumbukumbu ya Mzee Mandela.
 
Ban Ki-Moon Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, akipunga mkono kuwasalimu umati wa watu katika viwanja vya FNB Soweto Jijini Johannesburg katika hafla ya maombolezo ya msiba wa Mkombozi wa Taifa hilo.
 Raia wa Afrika ya kusini akisherekea kwa pamoja katika msiba wa Mzee Nelson Mandela
 
asdasvzdfnbgdnfgnfg
 
Baadhi ya raia wa Afrika ya kusini katika sherehe za maombolezo ya kifo cha Madiba Mandela hii leo
  Muda mfupi baada ya kuwasili Rais Obama wa Marekani akipunga mkono usawa waskrini ya TV ikiwa ni ishara ya kusabahi umati, kushoto kwake ni mkewe wakiwa pamoja na wanaafrika kusini  katika hafla hiyo ya maombolezo ya msiba wa Mzee Nelson Mandela leo Jijini Johannesburg.
 Washabiki wa chama cha ANC wakiwa wamebeba picha kubwa kuonyesha ya Mzee Nelson Mandela aliyeikomboa nchi hiyo toka kwa makaburu.


Source Daily Mail.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment