STAA aliyetikisa mwaka 2013, Diamond amesema Wema ndiye mwanamke anayetamani kuwa naye katika maisha yake, hivyo kauli yake aliyoitoa mwanzo kuhusu kuzaa na Wema ipo mbioni kutimia.
Mkali huyo wa Ngololo aliimbia Mwanaspoti kuwa sifa za mwanamke anayemtaka Wema anazo ndiyo maana hakusita kurejea upya kwa mrembo huyo ili auridhishe moyo wake na kutimiza malengo yake ya kuzaa na supastaa huyo.
“Miezi kadhaa nyuma niliongea kuhusu nia yangu ya kuzaa na Wema, wakati huo nilikuwa bado na Penny, siwezi kukimbia kivuli changu kwani ukweli unabaki palepale nampenda yule binti, japokuwa wapo wanaosema kwamba sijatulia au natafuta ‘kiki’ kupitia warembo hawa, si kweli, Wema nilikuwa naye kabla ya Penny na vigezo vyangu ni mchumba anayejali kazi yangu na kujua kwamba mimi ni staa nahitajika sehemu yoyote, muda wowote, Wema ni mwelewa.”
Akizungumzia kuhusu kauli yake kwamba anahitaji msichana asiyejichubua kama alivyosema kwenye makala iliyochapishwa na gazeti hili Diamond alisema “Umemwona Wema, kwa sasa ana ngozi nzuri yenye afya na iliyo na mng’aro kama alivyokuwa awali, ameacha kabisa kutumia dawa za kung’arisha ngozi hilo ndilo lililonivutia zaidi kwani alisikiliza ushauri niliompa kabla.”
credt: mwanaspoti.
credt: mwanaspoti.
TUPE MAONI YAKO HAPA:

0 comments:
Post a Comment