Miaka kadhaa iliyopita, niligundua kwamba kijana mmoja wa wa mtaani kwetu anachezea timu ya watoto chini ya miaka 21 ya Serengeti Boyz na kwamba kijana huyo ana miaka 20 kwa kipindi hicho. Nilishtushwa, ila baadae nikaja kugundua kwamba kuna kitu kinaitwa 'miaka ya mpira.' Kama ukijaribu kuufichua ukweli watu wengi watakuchukia, watasema kuwa wewe ni "adui wa maendeleo". Hivyo, uongo unaendelea.

Je hii inaweza kuwa ni ishu ya Samuel Eto'o? Kila kitu kinawezekana. Inaonekana kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, ni mmoja kati ya watu ambao hawaamini kwamba Eto'o ana miaka 32. Kwa maneno ya Mourinho: "tatizo la Chelsea ni uhaba wa mfungaji. Nina Eto’o ila ana miaka 32, labda 35, nani anayefahamu?"

Ila aliyewahi kuwa mpenzi wake, Anna Barranca, mwenye mtoto wa kike wa miaka 11 aliyezaa na Eto'o amefunguka...

Mwanamke huyo mwenye miaka 34 amesema kwamba Eto'o hana mika 32 kama ambavyo amekuwa akisema ila ana miaka 39 kuelekea 40.
 

Hapo chini ni vile ambavyo Anna Barranca aliliambia gazeti la The Sun la UK: "Nadhani Samuel hana miaka 35 [kama Mourinho alivyodhani] ana miaka zaidi ya 39. Samuel alizaliwa mwaka 1974 hivyo inamfanya awe na miaka 39 sasa.' Anasema alielezwa juu ya umri sahihi wa Eto'o alipokuwa kwenye mahusiano naye na rafiki aliyekuwa pamoja na mchezaji huyo nchini Cameroon.
 

Kumbukumbu rasmi za Eto's zinaonyesha kwamba alizaliwa mwaka 1981. Sijui tumuamini nani?
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment