Shabaash! Jamaa ambaye jina halikupatikana
aliyedai kuwa ni mume wa mtu, ameonja joto ya jiwe baada ya kujikuta
akikunjwa na mwanamke kisa penzi la bure alilopewa akashindwa kulilipia.

Kama mshale, OFM ambao huwa hawalazi damu, walifika mara moja na kunasa tukio hilo lililokuwa ndani ya mgahawa ambao mchana huuza chakula na usiku ni danguro.
Katika tukio hilo ilionekana kuwa mwanaume alizidiwa kwani muda mwingi alikuwa amekunjwa kwa nguo yake shingoni na mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Frida.
“Huwezi kwenda hotelini ukala chakula bure. Lazima ulipe. Jamani huyu baba tumekubaliana nimpe huduma kwa shilingi elfu tano, sasa amemaliza shida zake hataki kunipa changu. Hii ni kazi kama kazi nyingine tuheshimiane,” alisema Frida kwa jazba.

Kwa upande wake, mwanaume alikuwa akiomba asipigwe picha kwani ni baba wa watoto wawili hivyo akitolewa gazetini ataonekana alichepuka.
“Naomba msinipige picha, nikitoka gazetini itakuwa aibu. Nina mke na watoto nitadhalilika,” alisema jamaa huyo.

Baadaye kila mmoja alichukua hamsini zake baada ya mwanaume huyo kuingia mitini kibabe bila kumlipa Frida.
NENO LA MHARIRI
Utafiti unaonesha kwamba watu wengi walio katika ndoa ndiyo wanaongoza kwa kusaliti hivyo wanandoa tafakarini halafu mchukue hatua.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment