ulinzi mkali  wakati  mbunge  Msigwa na  watuhumiwa  wengine  70  wakifikishwa mahakamani leo
 
 
 
 Wafuasi  wa  Chadema  na  wananchi  wakiwa  nje ya  geti la mahakama  leo


Watuhumiwa  70  wa vurugu  za machinga  na polisi mjini Iringa akiwemo mbunge  wa  jimbo  hilo mchungaji Peter  Msigwa hivi  sasa  wanafanyiwa  utaratibu  wa  dhamana  baada ya mahakama  kukubali  kupewa  dhamana  baada ya  kusomewa mashitaka matatu  huku mbunge  akisomewa mashitaka mawili likiwemo  kushawishi  na kufanya mkutano bila  kibali  .

Watuhumiwa  wote  wamekana  mashitaka  dhidi yao na kwa  sasa  utaratibu  wa dhamana  unafanyika mbele  ya mahakama  hiyo ya  hakimu mkazi  wa wilaya ya  Iringa Mheshimiwa  Godfrey Isaya .

Hata  hivyo wamekana  mashitaka  yote yaliyotolewa ambayo shitaka la kwanza la mbunge ni kushawishi kufanya vurugu  ,huku  wengine  wote  kosa la kwanza kufanya mkutano bila kibali , kuharibu mali kinyume na sheria ni  kufanya  vurugu .

Hadi  sasa baadhi ya  watuhumiwa  wana wadhamini na dhamana yao ni kusaini hati ya dhamana yenye thamani ya Tsh milioni 1 na  kuwa na mdhamini mmoja mwaminifu.

Habari kamili  inakujia hivi  punde  ila hadi  sasa  mdhamini  wa mbunge Msigwa na baadhi ya  watuhumiwa  waliowengi wametimiza masharti ya  dhamana.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment