Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao.
Washitakiwa hao waliokamatwa katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti.
Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.
“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.
Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.
Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa tena mei 28 mwaka huu,ambapo washitakiwa wote walipelekwa Segerea.
Wakati huohuo, jeshi la Polisi mkoa wa kinondoni , limewakamata watuhumiwa 716 waliokuwa wakijihusisha na biashara ya kuuza miili kati yao wanaume 38 na wanawake 678.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela, alisema watu hao walikamatwa kwenye msako uliodumu kwa miezi sita kwenye maeneo mbalimbali ya Kinondoni.
Maeneo hayo ni baa, kumbi za starehe, madanguro, sehemu za wazi katika ufukwe wa Bahari ya Hindi, na makaburini ambapo kati ya wanaume waliokamatwa wengine ni mashoga pamoja na wateja wa machagudoa.
“Msako huo ulifanyika Maisha Club, Coco Beach, Barabara ya Tunisia , Travertine Hotel, Tandale Uwanja wa Fisi, Ambiance Club, Shekilango pamoja na Mwinanyamala” Alisema
Kamanda Kenyela aliongeza kuwa , jeshi hilo pia limewakamata raia 12 kutoka nchini Ethiopia walioingia nchini bila kibali kati ya Mei 2 na 6, mwaka huu katika eneo la Kimara Mwisho na Tegeta Kibaoni.
Alisema kukamatwa kwao kulitokana na taarifa walizozipata kutoka kwa raia wema waliowaona maeneo.
SOURCE: MPEKUZI
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment