Kwa mujibu wa Mwana FA mwenyewe ambaye leo
 ameachia wimbo wake mpya, Kama Zamani, hivi
karibuni alipokea malipo ya miezi mitatu kutoka
kampuni moja ya kuuza miito ya simu aka RBT
yanayofikia shilingi za kitanzania milioni 18.
Akiongea leo kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM,
 FA aliyekuwa wa tatu kati ya wasanii waliopata fedha 
nyingi zaidi kwenye malipo hayo chini ya Rose Mhando 
na Diamond, amesema ameamua kuweka wazi hilo ili 
watu waondoe imani kuwa muziki wa hip hop hauuzi.
Tarehe 31 mwezi huu, Mwana FA ambaye jina lake 
halisi ni Hamis Mwinjuma atakuwa na show yake aliyoipa jina, The Finest.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment