MLIMBWENDE aliyejitosa kwenye tasnia ya filamu za Kibongo na kufanya vizuri, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ ameanzisha Kipindi cha Kidoti Time ambacho kitafundishwa katika shule za Msingi 27 Songea vijijni Mkoani Ruvuma.
Jokate hivi karibuni aliliambia Ijumaa kwamba lengo la kuanzisha kipindi hicho ni kuwahamasisha vijana kubaki mashuleni na kuwafanya wafurahie kile wanachofundishwa huku wakikuza vipaji vyao na kutimiza ndoto zao.
Mbali na hivyo, Jokate alisema kipindi hicho kitawafundisha vijana hao uvumilivu, usikivu na kutambua kwamba elimu ndiyo mkombozi wao.
“Wanafunzi wengi wa vijijini wamesahaulika, wengi wao wanakata tamaa ya kuendelea na shule kwa kukatisha masomo yao. Kipindi changu kitawapa moyo na kuwafanya waipende shule na kujitambua kuwa hakuna kitu kilicho bora kama elimu,” alisema Jokate.

TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment