Katika pati hiyo iliyofanyika maeneo ya Leaders, Kinondoni, Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, mbali na mashoga hao waliokuwa wakiserebuka taarab, pati hiyo pia ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali ambao walimtuza Anthonio fedha na zawadi kibao.
Akipiga stori na Risasi Mchanganyiko, Sara alifunguka kuwa alifurahishwa na tukio hilo la mwanaye kutimiza umri huo kwani malezi si mchezo, yanahitaji kujipanga.
Sarah alimzawadia mwanaye simu aina ya Ferrari yenye thamani ya Sh. laki tano huku maandalizi yote ya shughuli hiyo yakigharimu Sh. milioni 3.
Wageni waliomtuza mtoto huyo ni pamoja na Faiza ambaye ni mzazi mwenza wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na muuza nyago kwenye video za wasanii wa Bongo Fleva, Mimah Mohamed ‘Baby Candy’.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment