Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kumtia mbaroni mzee wa mika 65 aliyembaka binti wa miaka sita anayesoma chekechea.
Kwa mujibu wa mkuu wa Polisi wilayani Kahama George Simba amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo May 19 mwaka huu saa 12 jioni eneo la Majengo wilayani Humo.
Akiendelea kufafanua Simba amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Mageta Singu anayefahamika pia kwa jina la Babu kabila msukuma kazi ni mkulima ambaye ni mkazi wa Majengo wilayani Kahama.
Imeelezwa Baada ya kufanya kosa hilo mtuhumiwa alitokomea kusikojulika ambapo jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wananchi waliendelea na msako hadi kufanikiwa kumkamata leo asubuhi maeneo ya majengo wilayani humo.
Kwa mujibu wa Kamanda Simba amesema kuwa kwa sasa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi kwa mahojiano na jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na pindi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la ubakaji.
Kutokana na matukio ya ubakaji kuwa mengi Wilayani Kahama,Jeshi la Polisi wilayani humo kupitia dawati la Jinsia limeweka mikakati thabiti ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa mabinti na wazazi kwa ujumla ili kujua na kuviepuka vyanzo hatarishi vya ubakaji.

TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment