Watangazaji wa Nuru FM kutoka kushoto Shadrack Mwansasu na Yusta Msowoya kulia wakimpa pore mtangazaji mwenzao Husein Farahan ambae leo alikamatwa na polisi wakati akielekea kazini na kuchezea kipigo na kuwekwa rumande
Mwili wa mtangazaji Husein Farahan ukiwa umevimba baada ya kichapo kutoka kwa askari wa FFU leo
Kichapo kilikuwa kikali kweli asimulia mtangazaji huyo
Mtangazaji wa kituo cha Nuru FM Husein Farahan amesimulia kilichomkuta kuwa alikuwa katika usafiri na boda boda na kusimamishwa na polisi kabla ya kuchezea kipigo Mtangazaji huyo alisema kuwa alikamatwa eneo la Mshindo baada ya askari hao kumsimamisha na kuanza kutembeza kipigo na kuwa amepatwa na majeraha mgongoni kutokana na kupigwa virungu mtindo mmoja. Hata hivyo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda amesema kuwa mbali ya mtangazaji huyo kukamatwa pia wapo askari polisi waliokamatwa kutokana na kutofahamika na kuwa askari hao ni wanachuo ambao wapo mjini hapa kimasomo japo kwa sasa wameachiwa huru. Kamuhanda amesema kuwa waliokamatwa hadi jana saa 3 usiku walikuwa ni watu zaidi ya 100 na kuwa baadhi yao wameachiwa na wanaoendelea kushirikiliwa ni 80 na leo asubuhi wangefikishwa mahakamani . |
0 comments:
Post a Comment