Leo wakati nakuja hapa nilipo muda huu nilikuwa nimeongozana na wadada kama
 wa-4 hivi inaonekana wanaishi jirani na wanakofanyia kazi au wanakoishi ni kumoja.

Wadada hawa walikua na story iliyovuta masikio yangu na kunifanya nipunguze spidi ili 
niendelee kuwasikiliza kwa kuwa tulipokuwa pana ka umbali kidogo hadi ufikie kituo cha
 usafiri wetu wa umma[Hiace/daladala/vifordi] 

Wadada hawa walikuwa wanamzungumzia mwenzao ambae inaonekana siku za
 karibuni ataolewa.
Tatizo hapa halikuwa kuolewa bali anaemuoa.

Inasemekana kuwa huyo mume mtarajiwa wa rafiki wa hao akina dada hajawahi kufanya   
ngono,yaani ni bikra wa kiume.


  Wadada wale walikuwa wanamlaumu mwenzao kwa kutokusikiliza maelekezo
 yao kwa
 kukataa kuolewa na huyo jamaa kwakuwa ni "mshamba" yaani hayajui
 mapenzi kitendo kitakachomfanya rafiki yao aanze kutembeza shule kwa huyo 
mume namna ya kugegeda 
kitendo ambacho wale wadada hawakukubaliana nachoWalionekana kukerwa sana na
 walikuwa wanasema wao hawawezi kuja kuolewa au kuwa na mahusiano na mwanaume
 wa aina hiyo.
  
Story hiyo ikanikumbusha miezi kadhaa iliyopita nilikuwa nazungumza na jamaa zangu
 kuhusiana na suala hili ambapo kuna jamaa alikuja kutulalamikia kuhusiana na mkewe
 kutokujua mapenzi kwa sababu alimkuta bikra.
  
Jamaa yetu yule alionekana kukereka sana na alifikia kusema kama angejua asingemuoa. 
Kati ya vijana tuliokuwa pale watatu walikubaliana na yule jamaa. 

Nilishangaa!Nilidhani kuwa kama ukimkuta mwanamke sio used basi unafurahi kumbe
 sio. 
 
Sasa nikiunganisha na hili tukio la leo naona hili jambo kama linakua flani hivi,yaani huenda 
hili suala hapo siku za nyuma lilikuwepo lakini inaonekana linachukua kasi mbaya. 
Nimeamua kulileta hapa ili nijue Wanaume wa hapa wanalichukuliaje suala hili. Pia
 wanawake nao wanalichukuliaje hili. 
 
Yaani kama kuna watu wawili ambao unatakiwa uchague kati ya huyo mmoja awe
 mwenzi wako na mmoja ni used na mwingine sio,ungependa yupi awe mwenzi 
wako na kwanini?
  
Watu wa siku hizi inaonekana hawapendi masuala ya kuanza kufundishana,wanataka 
watu ambao ni waalimu tayari.Inaonekana sisi mabikra tutaipata mwaka huu....lol! 

Naomba mchango wako tafadhali!  
-Mdau






LIKE PAGE YETU HAPA UWEZE KUPATA HABARI ZAIDI
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment