Julieth Samson a.k.a Kemmy ambaye ni mmoja kati ya waasisi wa Kaole Sanaa Group kutokana na kuwa mmoja wa wasanii wa mwanzo mwanzo kabisa katika kikundi hicho.
Mbali na uigizaji, Kemmy ni CEO wa Giligali Entertaimant Co Ltd ambayo inajihusisha na utengenezaji wa muvi ambapo hadi sasa imeshafanya filamu kama vile ‘NGUVU YA IMANI’, ‘BEST COUPLE’ n.k.

Kwasasa , Kemmy anajihusisha na maswala ya uinjilisti pia lakini sio sababu ya yeye kuachana na uigizaji, kitu kilichosababisha BK imtafute na kulizungumzia jambo hilo, anawezaje kumudu kazi zote mbili kwa wa wakati mmoja?
“Kwa kweli mimi mwinjilisti safi na namtumikia Mungu kwa moyo wangu wote ijapokuwa watu wengine wanadhani kwamba mtu akiwa mwinjilisti au ameokoka basi anaacha kila kitu cha dunia, hapana, mimi namtumikia Mungu na bado nafanya filamu. Pia ninaipenda sana kazi yangu, nikiambiwa kucheza sehemu yeyote nacheza coz nipo kazini kama alivyo mtu mwingine, maneno ya Mungu yanasema asiyefanya kazi na asile so bado naigiza kwa scene ninazoona zinampendeza Mungu.” – Kemmy
LIKE PAGE YETU HAPA UWEZE KUPATA HABARI ZAIDI
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment