Hili suala ni gumu kuliko linavyofikirika na jamii na watu ambao hawajapatwa na mikasa migumu. Ndio maana unyanyapaa unaendelea kutawala sana humu nchini na tatizo linazidi kushamiri. Nilikuwa na mchumba ambaye nilimpenda sana na ndiye niliyemuweka kuwa chaguo langu la maisha.
Mwanzoni mwa uhusiano wetu tulikuwa tukifanya mapenzi kwa kutumia condom na baadaye tulikuja kuacha kutumia baada ya kupima several times na kuona tupo vizuri na tulikuwa tumeshakubaliana kuja kuishi pamoja. Nilimtambulisha kwa ndugu zangu kama ndiye ndugu yao atakayeongezeka na yeye alinitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake.
Miaka ilivyozidi kwenda niliona mabadiliko kwa mwenzangu kitabia kwani kuna wakati alikuwa akinidanganya kwamba amesafiri kumbe yupo na hajaondoka. Kumbe mwenzangu alishaanzisha uhusiano na wazee wa mujini wenye pesa zao hivyo akawa ananipotezea kwani kwa wakati huo ndo nilikuwa namalizia mwaka wangu wa mwisho chuoni.
Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kwani ilifika kipindi akanambia ile mipango tuisitishe. nilipomuuliza kwa nini, hakuwa na jibu la wazi. Ilinichanganya sana lakini nilipata faraja kutoka kwa rafiki zangu na ndugu nikatulia. Baada ya miezi kama sita kupita niliamua kwenda kupima na nikagundulika kwamba niko na maambukizi ya VVU, nilichanganyikiwa sana na niliona kama hakuna haja ya kuishi tena.
Sikumwambia mtu mwingine zaidi ya doctor mmoja na mimi mwenyewe kuugulia maumivu yangu peke yangu ila kuna wakati ndugu na jamaa walikuwa wakiniona nimebadirika ila nawaambia hakuna shida yoyote na nipo kawaida. Nilijitahidi kutokukaa peke yangu kwani mawazo ndo yangenizidia.
Mpaka sasa hivi nipo vizuri na nna afya njema ila napata wakati mgumu sana kwani wasichana wengi wanaonesha dalili za kutaka kuwa na uhusiano na mimi lakini nawaonea huruma sana kwani inaniuma sana nikifikiria kumwambukiza mtu mwingine. Wengi wao nimekuwa nikiwakwepa mpaka wengine wananitangazia kwamba jogoo wangu hawiki, huwa inaniuma sana kwani sitaki wajue na sipendi kuwafanya wawe kama mimi.
Nisiwasumbue sana, naomba nihitimishe kwa kusema; hili tatizo ni gumu sana hasa unapokuwa wewe ndiwe 100%. Tupigeni vita unyanyapaa ili watu wasiwe na mawazo ya kwamba TUFE WENGI. Pia unayemnyanyapaa hujui aliupata vipi kwani si kila mwenye VVU alikuwa kuruka njia. Kuna wengine wameupata kutoka kwa watu wanaowaamini sana! Na wengine miaka ya leo wamezaliwa nao hivyo sio kosa lao kwa hapo walipo.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment