Msanii wa filamu nchini, Steve Nyerere amesema amepata mwaliko wa kwenda kuhojiwa na shirika la habari la Uingereza, BBC kutokana na kufanya filamu za kumuenzi Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
CIMG3117
Steve alisema anatarajia kwenda kufanya show London mapema mwakani pamoja na kuhudhuria mwaliko wake BBC.
“Nipepata bahati ya mwaliko mzuri wakualikwa na kituo cha BBC London,kama Steve Nyerere ninayemuenzi Nyerere katika filamu,nadhani mwezi wa kwanza Mungu akinibariki nitaenda,” alisema Steve.
“Kuna kampuni ambayo inanisimamia kazi zangu zote za filamu na kunitangaza kimataifa hata show ya London wao ndio wamenitafutia na pia kuna mambo mengine mengi ambayo yanakuja kwa jinsi walivyoniambia. Nimeona umuhimu wa kumuenzi Mwl Nyerere kwasababu bado kuna watu na watoto wanataka kujua Nyerere ni nani na alifanya vitu gani,kama mimi nitahakikisha kila mwaka ninatoa filamu moja ambayo itakuwa inaelezea mambo mbalimbali na hotuba zake.”
LIKE PAGE YETU HAPA UWEZE KUPATA HABARI ZAIDI
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment