KANISA Katoliki limeingia kwenye kashfa baada ya mmoja wa mapadri wake katika Jimbo Katoliki Singida, Deogratius Makuri kufikishwa kwenye Mahakama ya Mwanzo Utemini mjini Singida, akituhumiwa kushindwa kutunza mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Ferdinand Njau, ilidaiwa, kuwa Padri Makuri alikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na Maria Boniphace (26) ambaye alikuwa mhudumu katika jimbo hilo.
Ilielezwa kuwa katika kipindi cha uhusiano wao, Padri Makuri alimpa mimba mtumishi wa jimbo hilo, Maria. Maria aliiambia Mahakama hiyo kuwa mara alipopata ujauzito, aliwaarifu wazazi wake ambao walimwendea Padri na alikubali kuhusika na ujauzito wa binti huyo.
Ilidaiwa kuwa Padri aliahidi kwa maandishi kuwa atatunza mtoto atakayezaliwa hadi atakapokuwa na uwezo wa kujitegemea.
Maria aliendelea kudai kuwa Padri Makuri alitekeleza ahadi yake hiyo kwa miezi michache tu kisha akasitisha huduma hiyo ya kumpa mwanawe matunzo.
Alisema baada ya hapo, alimfikisha Padri huyo Idara ya Ustawi wa Jamii ambapo katika hati ya mkataba, aliahidi kuwa atakuwa anatoa Sh 80,000 kila mwezi na iwapo atashindwa kufanya hivyo, afikishwe mahakamani mara moja.
Hata hivyo, pamoja na ahadi hiyo, Padri Makuri alianza kudai mtoto huyo si wake, hivyo akaamua kuacha kutoa matunzo.
>>Habari leo
>>Habari leo
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment