Muimbaji na mtayarishaji huyo wa muziki aliiambia tovuti ya Times FM kuwa ugumu wa ndoa umemfanya asifikirie tena kuoa maishani.
“I’m single, sitaoa tena…mimi niko single na sitaoa tena. Kwa sababu nimeona ugumu wa ndoa na wepesi wa kuwa bachelor. Kwa hiyo nimeamua kuwa bachelor na siwezi kuoa tena, sioi tena jamani I’m single. No more kuoa Bob Junior,” aliiambia tovuti huyo.
“Unajua unapokuwa kwenye mahusiano ya boyfriend na girlfriend, hamna ile ‘uko wapi sasa hivi, rudi haraka nyumbani’, umeenda kwenye show ukirudi mara kanuna.”
Bob Junior aliiambia tovuti hiyo kuwa ndoa yake ilikuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya kazi yake kwa kuwa katika siku saba za wiki ni siku mbili tu anakuwa na furaha, na kwa kuwa kazi yake inategemea ubunifu na utulivu asingeweza kufanya kazi vizuri.
Alisema mkewe alikuwa na wivu kiasi cha kuiingilia hadi ukurasa wake wa Facebook na kuwatukana watu waliokuwa wanachat naye.
Bongo5
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment