HUKU akiendelea kukanusha kutibua ndoa ya shoga’ke kwa macho makavu, mwigizaji wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja hivi karibuni amenaswa laivu akila bata na mume huyo wa shoga’ake huko nchini China.
Kajala (kulia) akila bata na mume wa shoga yake nchini China.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Kajala amenaswa akijiachia kwenye kumbi mbalimbali za burudani nchini humo sambamba na mwanaume huyo.
“Huyu mwanamke amewadanganya mashoga zake na ndugu zake huko Bongo kwamba amekwenda Zambia, mbona anaonekana huku akila bata na mume wa Sabrina?” kimehoji chanzo chetu.
“Huyu mwanamke amewadanganya mashoga zake na ndugu zake huko Bongo kwamba amekwenda Zambia, mbona anaonekana huku akila bata na mume wa Sabrina?” kimehoji chanzo chetu.
Chanzo hicho kimeendelea kudai kwamba Kajala anatanua na mume wa shoga’ke huyo aitwaye Sabrina Kimaro bila ya kuona haya.
Kajala Masanja.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Sabrina alisema kuwa hivi sasa kama amechanganyikiwa kwa kuwa kila siku anakunywa pombe ili kupoteza mawazo ya kuporwa mume na shoga’ake kitu ambacho hakukutegemea maishani mwake.
“Kwa kweli naumia sana, awali kuna baadhi ya watu waliamini kuwa nilikuwa natafuta umaarufu kwa kumsingiza Kajala, sasa kila mtu anaona kuwa ni kweli, naamini Mungu atanilipa,” alisema Sabrina.
Gazeti hili lilifanya juu chini kumtafuta Kajala ili kuweza kujua undani wa kitendo hicho muda mchache baada ya kuinasa picha yake akiwa na mume huyo wa Sabrina.
Gazeti hili lilifanya juu chini kumtafuta Kajala ili kuweza kujua undani wa kitendo hicho muda mchache baada ya kuinasa picha yake akiwa na mume huyo wa Sabrina.
“Niko Rufiji nimekuja kushuti filamu,” alisema Kajala.
Katika kuthibitisha hilo, mwandishi wetu alimtafuta rafiki wa karibu wa Kajala (jina kapuni) ambaye alikiri kwamba msanii huyo amemuaga bwana wake wa Dar kwamba anakwenda Zambia kununua vifaa vya kurekodi filamu.
“Hata miye nimeshangaa kusikia kuwa yuko China,” alisema shoga huyo.

TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment