Kwa miezi hii yote ilikua inajulikana Feza yupo Botswana kwa O’neal ambae headlines zilitangaza sana kwamba mapenzi ya wawili hawa yanaweza kuwafikisha mpaka kwenye ndoa.
Sasa basi, mchapo wa leo ni kuhusu info mpya Exclusive on millardayo.com kwamba Feza ameondoka Botswana na kuhamia South Africa ili kujijenga zaidi kimuziki na pia kujitangaza na kuutangaza muziki wenyewe wa bongofleva anaoufanya.
Swali la kwanza nililomuuliza baada ya kusema kahamia SA lilikua >>> Umehamia South Africa na boyfriend wako? akajibu ‘No, niko mwenyewe lakini na yeye kahamia sio mbali sana na hapa, ni majirani’
millardayo.com : Umehamishia makazi yako huko moja kwa moja? akajibu >>> ‘Hapana, nitakua part time huku na time nyingine Tanzania’
millardayo.com : Na Boyfriend wako kahamia moja kwa moja South Africa? akajibu >>> ‘Na yeye ana mazungumzo na Radio Stations za huku so atahamia moja kwa moja, sijui zaidi ya hapo’
Hii picha ya juu ni wakati Feza alipowasili Botswana kwa kina O’neal.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment