Adha hii imempata mwanamke huyu baada ya kuanza kuona ngozi yake imeanza kuwa laini kasi kwamba alianza kumomonyoka taratibu mwisho wa siku alijikuta ameoza wanawake wengi huwa wanajikuta wanaingia katika taabu hizi kwa kufuata mkumbo

Dawa za kuongeza makalio zina madhara kwa mtumiaji

 Hivi karibuni kumeoneshwa video katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo inaelezea madhara ya taratibu anayoyapata mwanamke aliyeongeza ukubwa wa makalio, kwa dawa za silkoni.
Video hiyo imeonesha kuwashtua wanawake wengi waliowahi kutumia aina yoyote ya dawa hizo.
 Taarifa hiyo imeeleza kuwa, dawa hizo badala ya kumfanya mwanamke awe laini, video hiyo inaelezea namna ukuaji wa haraka wa makalio pamoja na kuathirika huku yakiachwa katika sura mbaya sehemu za nyuma (chini) baada ya muda mfupi.
Imebainika kuwa, pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa makalio ya akina dada kupendwa, dawa hizo pia zina madhara kwa afya ya binadamu, ambapo wataalamu wa mambo ya afya wanadai kuwa, pamoja na kuongeza ukubwa wa makalio pia dawa huleta matatizo ya kuvimba kwa ngozi ya makalio katika mpangilio usio sahihi.
 Dawa hizo pia zimetajwa kuwa husababisha kwa uwepo mkubwa wa ugonjwa wa  saratani. Video hiyo ya sekunde 20, inamwonesha mwanamke aliyeongeza makalio yake kwa dawa za silicone akionyesha namna alivyoathirika kutokana na matumizi ya dawa hizo huku akisema kuwa, "Hivi ndivyo nilivyoongeza ukubwa wa makalio yangu." Na kuongeza kuwa, "Sidhani kama ni sahihi kufanya hivi. Nadhani kuna ulazima wa kuyaondoa haya makalio yangu yote kwa sasa."
Mtumiaji mmoja wa mtandao wa mawasiliano wa kijamii wa fasebook kutoka nchini Marekani Donna Wright-Levy, amechangia kwa kusema kuwa, "Mimi hupendelea kwenda maeneo kadhaa ambako hutengenezwa shepu yangu kwa dawa hizi sasa nina ulazima wa kwenda kupima saratani".
 Mmoja wa madaktari kutoka kliniki ya upasuaji ya BAAPS Aurora nchini Uingereza, Dk Adrian Richards, ambaye ni mshauri wa upasuaji anaamini kuwa mwanamke huyo amefanyiwa marekebisho ya makalio yake kwa dawa za silicone na kusema kuwa, tatizo hutokea wakati nyama ya makalio inaposhindwa kuulinda vema mwili na kuwa imara katika nyama na mifupa, hivyo madhara huanza kutokea juu ya ngozi na kusambaa mpaka ndani ya nyama na baadaye mfupa
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment