Mkuu wa Idara ya Uendeshaji kutoka Tigo Tanzania Bw. Deon Geyser akionyeshea  waandishi wa habari tuzo ya mtandao bora wa mwaka 2013 walioshinda kutoka kwa umoja wa makampuni ya simu GSMA katika kongamano la mawasiliano na mitandao ya simu Africa Com, iliyofanyika Capetown Afrika Kusini mwezi Novemba. Kushoto ni Mkuu wa Mipango na Uboreshaji wa mitandao kutoka Tigo Bi. Halima Idd..
Kampuni ya Tigo Tanzania imeshinda tuzo ya kuwa mtandao wa simu ulioboreshwa zaidi katika mwaka 2013 barani Afrika. Tuzo hiyo iliyotolewa katika kongamano la umoja wa makampuni za mawasiliano duniani, GSMA, liliyofanyika mwezi Novemba mjini Capetown, Afrika Kusini.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment