MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ hivi karibuni alimwaga machozi hadharani baada ya kuibiwa simu yake ya mkononi, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Kwa mujibu wa ‘sosi’ wetu aliyemshuhudia mwanadada huyo akilia, tukio hilo lilitokea Jumapili baada ya Shilole kushuka kwenye gari lake na kumwachia fundi kwa ajili ya marekebisho ambapo alipanda teksi na kuelekea saluni, alipofika akajikuta hana simu.
“Shilole alilia kama mtoto mdogo kwani alikuwa anatakiwa kusafiri siku hiyohiyo usiku kwenda Uingereza, ikabidi aanze kufanya jitihada za kupata simu nyingine lakini kwa kuwa ilikuwa ni wikiendi, kazi ilikuwa ngumu kwake,” kilisema chanzo hicho.
Mwandishi wetu alipojaribu kumtafuta Shilole ili aeleze simu ilikuwa ya gharama kiasi gani, hakuwa akipatikana hewani mpaka gazeti hili linaenda mtamboni.
SOURCE-GPL
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment