Siku moja baada ya wimbo mpya wa Ommy Dimpoz "Miss koi koi" kuvuja kwenye mtandao, Ommy Dimpoz amlalamikia producer "Manecke" kutoka AM Records na kudai yeye ndio atakuwa kaivujisha

"hata mi mwenyewe nimehangaa sana kwenye mitandao mara natumiwa meseji kwamba Ommy Dimpoz  amerelease nyimbo mpya...wengine wananitumia meseji mbona umerelease ngoma mpya ki-local local ghafla tu tunaona kwenye mitandao? kwahiyo mi nikasema hapana mbona mi sjiatoa hiyo nyimbo.
"hiyo nyimbo wakati wa tuzo za kilimanjaro ambazo nilipata awards zangu za kwanza za song ya Nainai, ndio kipindi ambacho katika wiki hiyohiyo nilikutana na Manecke na tuka plan kufanya kitu, i think ilikuwa ni 2012, nikaenda nikarecord nyimbo, unajua kama msanii unakuwa kila siku una record unarecord lakini baadae unaangalia labda planning nyimbo gani intoke, kwahiyo ilikuwa ina muda kidogo, hebu fikiria mpaka nimekuja kutoa  baadae me and you, tupogo na nilikuwaga sijawahi hata kuzirecord hiyo nyimbo ilikuwa tayari nimeshairecord."


"Mimi sasa nikaaamua jana kuidownload ile nyimbo na nilivyoicha studio niliiacha kama demo, lakini nilivyoi download naona kabisa kama ni nyimbo imeshamaliziwa kwa kiasi flani kwa kule mwisho, kwahiyo nikama nyimbo imeshafanyiwa mixing halafu mtu akaitoa, sasa kama mimi nimeacha nyimbo studio unategemea kwamba anaeitoa ile nyimbo ni nani? ni producer, huwezi ukasema labda aaaaaaah wanatoa wenyewe, mimi sikuwepo sikuwa na ile nyimbo! nimeitoa vipi sasa?."

Je aliongea na Manecke baada ya kusikia wimbo huo?
"ki ukweli hii ni kazi yangu na mimi ndio ninaitegemea,  kwamba ninavyofanya kitu flani nakua na mipango nacho, kwahiyo hata kama ningekuwa nataka kufanya hata hiyo nyimbo ningetaka iwe kubwa, ina maana ningetengenezea mipango iwe kubwa, lakini nimesikitika kiasi kwamba nimeshindwa hata kumpigia Maneke, sababu kama kitu kimeenda kwenye mitandao nikaona nami ni bora niandike kwenye twitter yangu kuwa Sija-release nyimbo yoyote tangu nilipotoa tupogo, lakini kuna nyimbo nimefanya miaka miwili iliyopita katika studio za AM reacord chini Maneke, na kama inavyolalamikiwa na wasanii wengine kuwa nyimbo zinavuja kutoka kwenye studio hiyo na nyimbo yangu pia imevuja."
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment