Nasibu Abdul Almaarufu kama Diamond Plutnum ni kati ya wasanii hapa nchini ambao wamekuwa wakionyesha upendo wao wa dhati kwa mama yake mzazi kiasi cha kuamua kuwa naye katika maeneo mengi hata anapopata nafasi ya kupiga show ndani na nje ya nchi kitu ambacho kimeonekana kukera baadhi ya mashabiki zake na kuhoji kuhusiana na hilo .
Alisikika mdau mmoja ambaye ni shabiki mkubwa sana wa msanii huyo diamond plutnum akihoji juu ya hali hiyo nakuonekana kukereka .
“unajua wasanii wengi sana wana mama zao na kila mmoja anampenda sana mama yake mzazi kwa namna moja ama nyingine lakini kwa upande wangu mimi nahisi kama nakwazika kwa hili la Diamond , maana kila mahali anaenda na mama yake hata katika shows anazoenda kupiga za usiku yupo na mama yake, sasa ndo kumpenda sana au ???” alihoji shabiki huyo
mbali na huyo yupo pia mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Subira Chacha ambaye yupo katika manispaa ya musoma naye alisema kitu kinachoboa zaidi ni tabia ya msanii huyo kuambatana na mama yake mzazi kila mahali.
“Diamond Plutnum ni msanii mzuri sana maana mi mwenyewe ni shabiki wake ila ananiboa kitu kimoja tu ,tabia ya kuambatana na mama yake mzazi kila mahali, duh, inaniboa kiukweli hata kama ni upendo huo wake umepitiliza.”alisema
Naye Blogger Wa Blog Ya Jicho La Mdadisi na ambaye pia ni mtangazaji wa Kituo Cha Radio Victoria Fm 90.6 Kilichopo Musoma Mara ,Bwana Ahmad Nandonde katika hilo yeye alisema haina tatizo isipokuwa sio utamaduni ambao umezoeleka sana kwa hapa nyumbani ndio maana wengi wanaboreka.
“sijaona kama ni tatizo kwa msanii huyu kuambatana na mama yake mzazi kila mahali ,lakini pia inabidi yeye mwenyewe awe anaangalia kama ni sahihi kwa upande wake au la , na pia unajua hili wengi linawaboa lakini ni kwaajili tu haijazoeleka kwa hapa kwetu msanii kuambatana hivyo na mama yake mzazi kila mahali na hasa katika shows zake.”alisema Ahmadi
Diamond Plutnum alipotafutwa kuhusianaa na hili hakuweza kupatikana kwasababu ambazo zilielezwa kuwa ndio alikuwa anarudi hapa nchini leo hii baada ya kupiga show yake huko nchini Kenya .
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment