Kila kukicha kuna wasanii wa maigizo na filamu ambao tunasikia
wamekamatwa na madawa ya kulevya, "unga" katika jitihada za 'kusaka maisha', wenyewe wanasema kuna ajali kazini. Wasanii hao ambao wengi ni vijana, na pale wanapoonekana kwenye runinga huwa hamasa kwa wadogo zao na jamii kwa ujumla, wakipenda kuwa kama wao.
Add caption |
Vijana wa Tanzania tuna shida gani? Kama ni ardhi tunayo, kama ni nguvu tunazo, sasa nini shida zaidi? Ipo haja ya Operesheni ambazo Askofu Sylvester Gamanywa ameitisha za Takasika iliyomalizika hivi karibuni, na kisha kupokelewa na Operesheni Milikisha, kuwahusisha pia wasanii wa aina zote, maana wanaonekana kukumbwa na janga hili kwa sana, vinginevyo, vijana ambao ndio nguvukazi ya taifa watakuwa wakijaa jela za ndani na nje, wakiacha wageni kuja kutawala.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment