Wazungu wanasema what goes around comes around. Picha linaanzaa miaka mtatu na kitu iliyopita, mitaa ya Mbagala jijini Dar es Salaam kwenye uchukuaji wa video ya wimbo wa pili wa Diamond uliompa mafanikio, Mbagala.
Katika scene ya mwisho pale Diamond anapoonekana kukaa chini akiwa amejiinamia kutokana na mawazo mengi aliyokuwa nayo kichwani, mara kama zali, anatokea msichana mrembo mwenye asili ya kiarabu akiwa amevalia gauni jekundu. Kwa haraka haraka kama wewe ungekuwa Diamond, kwa urembo wa msichana huyo ni rahisi kuhisi labda ni malaika aliyeshuka juu kuja kuziondoa shida zako muda huo. Msichana huyo anakaa alipo Diamond na kumshika mikono kumaanisha kuwa angependa awe tulizo la moyo wake kwa muda huo. Wawili hao Wanainuka na kuondoka.
Msichana huyo anaitwa Naima Shaa aka J.LO, anayedaiwa kuwa mtoto wa mbunge, Abdulkarim Shaa wa Mafia.
Kwa mujibu wa mahojiano tuliyofanya na Wema Sepetu kwaajili ya jarida letu la Mzuka mwaka jana, kipindi wanafanya video hiyo, ukaribu wa Diamond na Wema ulikuwa haujaanza. “Kipindi hicho mimi nilikuwa natoka na Chaz Baba so nakumbuka hiyo ndio ilikuwa the first and last day tumeonana. Mimi nikasafiri nikaenda Marekani, nilipofika kipindi hicho Kamwambie ndio ilikuwa hot na Mbagala ndio karelease,” Wema aliliambia jarida la Mzuka.
Hivyo ni ngumu kufahamu urafiki wa Wema na Naima ulikuwa kabla ya kuanza kwa uhusiano wa Wema na Diamond ama baadaye. Lakini inawezekana pia baada ya Naima kufanya video na Diamond, bado waliendelea kuwa karibu kiasi ambacho baada ya Diamond na Wema kuwa pamoja kama mtu na mpenzi wake, Naima akawa na ukaribu na Wema kupitia uhusiano huo wa kikazi na hitmaker wa Mbagala.
Wema na Naima waliendelea kuwa marafiki kwa kipindi kirefu na hata kama ukiangalia picha za Instagram za akaunti ya Naina, utaona walikuwa karibu bado.
Marehemu Sharo Milionea akiwa na Wema na Naima
Lakini sasa meza zimebadilika. Kwa mujibu wa tetesi za mtaani na pia gazeti la Ijumaa Wikienda likiweka msititizo, ni kwamba Naima na aliyekuwa mpenzi wa Wema, anayefahamika kwa jina la Clement ni wapenzi. Clement ndiye aliyekuwa mwanaume nyuma ya maisha ya kifahari ya Wema aliyemnunulia magari yake, kumpa nyumba, kumfungulia ofisi (vitu ambavyo tayari inasemekana amenyang’anywa kutokana na Wema kuendeleza uhusiano wake na Diamond).
Kwa mujibu wa chanzo kinachodaiwa kuongea na gazeti hilo la udaku la kampuni ya Global Publishers, Clement ameamua kutembea na Naima ili kumuumiza roho Wema. “Unaambiwa nyuma ya pazia stori ni kwamba anataka Wema aumie ndiyo maana ameamua kubanjuka na Naima huku akijua kabisa kuwa ni marafiki,” gazeti hilo limekinukuu chanzo hicho.
Tayari kuna picha ya Naima inayomuonesha akiwa amejichora tattoo yenye jina la Clement.
“Naima naye amedata kabisa na sidhani kama anaogopa Wema kujua kama yeye ndiye hasa anatembea na kigogo huyo kwa kipindi hiki,” chanzo hicho kilinukuliwa na gazeti hilo. Hata hivyo Naima amekanusha kwa kudai kuwa tattoo hiyo inamaanisha ‘Element’ na sio ‘Clement’.
Gazeti hilo linadai kuwa Wema haumizwi na wawili hao kuanzisha uhusiano kwakuwa tayari yupo na mtu anayempenda kwa dhati. “Moyo wangu ulishatulia kwa nimpendaye, nawatakia maisha mema,” Wema anadaiwa kuliambia gazeti hilo.
Kinachoifanya drama hii inoge, ni kwamba Naima naye ni mke wa mtu ambaye tayari ameingia kwenye mgogoro kwa kusaliti ndoa yake. “Unajua hata Naima ameingia kwenye gogoro la kindoa na mumewe kwa muda mrefu. Kisa ni huyo CK.”
Picha zaidi za Naima
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment