Kuna sababu nyingi za ndoa/mahusiano kuzifanya kuwa mbaya,lakini mojawapo ya tatizo ambalo linazisumbua ndoa nyingi ni kutokuwa na uhakika wa tendo la ndoa.Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa katika nyumba nyingi,liko tatizo la uhakika wa tendo la ndoa.Kuna wanawake kwa wanaume,wamekuwa wakiwanyima tendo hilo wapenzi wao kwa sababu mbalimbali.Ukweli ni kwamba ikiwa unamfanya mpenzi wako asiwe na uhakika wa tendo hili,jua unaiharibu ndoa yako mwenyewe.
Hata kama mwenzi wako ni mwema kiasi gani,kama unataka kuthibitisha ubaya wake mnyime.
Pia tafiti nyingi zinaonyesha kuwa kwa sababu ya kutokuwa tayari kwa baadhi ya wanandoa ktk tendo hilo,baadhi yao wamekuwa wakiona njia sahihi ni kutoka nje kusaka watu wengine ambao watakuwa tayari.
"Ni upuuzi,eti niko kwenye ndoa,mke wangu amekuwa akiniambia acha kunisumbua,jana tu nimekupa na leo unataka tena,kwani mimi ni mbwa,tena hata mbwa huwa anapumzika,niache bwana nilale"....Anasema mwanaume mmoja akilalamikia kitendo cha mkewe kumnyima.
Kwa ujumla wanaume ndio kundi linaloongoza kwa kunyimwa,kiasi kuwa baadhi yao wamekuwa wakitumia nguvu na hata kupiga makofi wake zao wakiwalazimisha wafanye kile ambacho wanataka.
Ukweli ni kuwa wanawake wanaponyimwa,si wengi wanaouchukua hatua mbaya kama hizi za kupiga au kwenda kwa wengine,ingawa taarifa za karibuni zinaonyesha kuwa wameanza kubadilika na kusaka wanaume wanaoweza kuwapa wanachotaka.
Amka ndugu yangu,fanya mambo yenye kuweza kukusaidia kuwa na ndoa kweli,ndoa ambayo mwanaume au mwanamke anajua wajibu wake na kuutekeleza.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment