KUNDI la watu ambao inadaiwa kwamba wamekula yamini ya kumchafua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kwa namna yoyote ile, wamemuonjesha machungu Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige.
Zitto, baada ya msululu wa tuhuma ambazo nyingi zilibainika kupikwa makusudi ili kuichafua taswira yake mbele ya jamii, sasa hivi anahusishwa kutoka kimapenzi na Magige, ikidaiwa kuwa walisafiri pamoja kwenda Dubai kwa ajili ya kufanya mambo yasiyofaa.
Hata hivyo, uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa tuhuma hiyo ya Zitto na Magige ni nyingine kati ya zile zilizopikwa, kwani ukweli wake ni wa kufikirika.
Imebainika kuwa safari ya Dubai ambayo inasemwa kuwa Zitto na Magige walisafiri, inapotoshwa kwa sababu ukweli ni kwamba wabunge hao walisafiri pamoja na timu nzima ya Kamati ya Hesabu za Serikali Bungeni (PAC) kwa shughuli za kikazi na hakukuwa na suala la mapenzi kati yao.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.
Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe, aliye makamu mwenyekiti wa PAC, akiizungumzia skendo hiyo ya Zitto na Magige alisema: “Nimeona ujumbe ambao unasambazwa kuhusu Zitto na Catherine (Magige), ni uongo mkubwa, hakuna kitu kama hicho.
“Nimeona wanazungumzia zaidi tiketi, ni kweli tulisafiri kamati nzima kwenda Dubai. Wajumbe wote wa PAC tulikwenda Dubai baadaye Uingereza. Zitto ndiye hakwenda Uingereza, yeye aliishia Dubai na kurudi nchini.
“Katika hili namsikitikia zaidi Magige kwa sababu anaingizwa kwenye vita ambayo haijui, siyo mzoefu wa kashfa hizi za kuzushiwa, Zitto angalau naweza kusema amezoea. Nitasimama kokote kumtetea Catherine na hata Zitto. Hili limeandaliwa makusudi kumchafua Zitto na hii ni vita ndani ya Chadema wao kwa wao.”
Mjumbe wa PAC, Esther Matiko, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Mkoa wa Mara, alisema: “Hilo suala ni la uongo kabisa, walioanzisha hiyo tuhuma  pengine wanataka kumchafua Catherine. Tulifikia hoteli moja na chumba changu na kile cha Catherine, vilikuwa karibukaribu, hakuna kitu kama hicho kinachosemwa.
“ Catherine alisafiri na mwanaye wa kike anayesoma kidato cha kwanza, na alikuwa akilala naye chumba kimoja, sasa hayo mambo yangewezekanaje? Hizi ni siasa tu. Kwanza Catherine hii siyo safari yake ya kwanza, kila tunaposafiri kwenda nje, huwa analala chumba kimoja na dada Lucy (Owenya, Mbunge wa Viti Maalum Chadema).
“Kitendo cha kupendelea kulala chumba kimoja na dada Lucy maana yake hapendi hayo mambo, tena ni kuonesha anaogopa manenomaneno kama haya. Safari zote huwa analala na dada Lucy, kasoro hiyo tu ndiyo alilala na mwanaye wa kike. Zaidi ya hayo, namsemea Zitto, yeye ni mwenyekiti wetu, amekuwa akitaka tuwe na maadili ndiyo maana hajawahi kuwa na uhusiano na mjumbe yeyote.”
Zitto hakupatikana kuzungumzia tuhuma hiyo lakini Catherine alipopatikana alisema kuwa hana maneno kwa sababu anajua kinachosemwa ni uongo, akaongeza: “Wanatishia wana video, waiweke wazi kama ni kweli. Hizi siasa za kuchafuana kwa vitu vya uongo hazifai hata kidogo, haziisaidii nchi.”
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment