Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa jijini Dar es Salaam jana.
Rais wa Shirikisho la Soka (TFF), Jamal Malinzi amesema shirikisho hilo limepanga malengo ya muda mfupi na mrefu ikiwa na sehemu ya mkakati wa kuendeleza na kuinua kiwango cha mchezo huo nchini.

Malinzi alieleza mikakati hiyo ya uongozi wake wakati alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana.
Alisema uongozi wake umepanga malengo hayo ikiwamo kuandaa mashindano maalumu ya kutafuta vipaji mikoani ili kuondokana na mtindo wa timu ya Taifa (Taifa Stars) kuundwa na wachezaji kutoka katika klabu chache tu.

Kwa upande wake Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), ameelezea matumaini yake kwa uongozi mpya wa TFF katika kuunga mkono juhudi za Rais Jakaya Kikwete katika kuimarisha na kuinyayua Tanzania katika ramani ya soka duniani. 
CHANZO: NIPASHE
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment