NAWASALIMU wasomaji wote wa  safu hii, nina hakika wote wazima na mnaendelea vema na maisha.
Kuna baadhi ya wanawake wana tabia kwamba kama mume ana fedha basi mapenzi huwa motomoto na anatamani amuogeshe lakini akiwa hana, ndoa inayumba.
 
Nawaambia wanawake wenye tabia hiyo kuwa kwani wazazi, kungwi na  majirani hawakukufunda kuwa ndoa inahitaji uvumilivu?


Hukufundwa kuwa mume kama hana fedha fanya biashara halali? Inaruhusiwa, mbaya ni kutoka nje ya ndoa lakini kujituma kwa ujasiriamali ili kumsaidia mumeo inawezekana.
 
Mumeo kama hana fedha na amefukuzwa kazi msaidiane kutafuta fedha kihalali kwa kuwa wajasiriamali.
 
Nikija upande wa pili, kuna baadhi ya wanaume wanapenda kulelewa, ukumbuke kuwa mwanaume ni wajibu wako kumtunza mkeo.

Wapo baadhi ya wanaume wanakuwa na fedha lakini wanatumia na nyumba ndogo na nyumbani anataka ahudumie mkewe hasa akijua kuwa ana fedha!
Wengine hudiriki kutelekeza watoto na kumuachia mkewe ahangaike nao.

Akiambiwa anakuwa mkali, huo ni ukatili hasa kama una fedha lakini haijulikani unazitumiaje.
Wapo wanaotegemea biashara za wake zao wao kazi yao ni kujichana na nyumba ndogo, je huo ni uungwana kweli?

Wewe mume tegemezi hiyo si tabia nzuri, mwanamke anataka mapambo, mbona wa wenzio ukiwaona wazuri unawatamani wako unamfuja? Halloo iwaingie akilini wote wenye mapenzi ya pesa!
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment