ILE Oparesheni Fichua Maovu (OFM) safari hii iko kimataifa zaidi ambapo wiki iliyopita ilitua huko Hong Kong, China na kunasa ufuska wa wanawake wa Kibongo wanaokwenda nchini humo kwa kigezo cha biashara kumbe wanakwenda kuuza miili.
OFM ilipata taarifa kutoka kwa chanzo chake ndipo ikatuma kachero wake nchini humo na kujionea vitu vinavyochafua taswira ya Tanzania nje ya nchi hasa China kama wanadada hao wanavyofanya uchafu tena wengi wao Bongo ni mastaa.
“Kiukweli ni aibu! Wanawake wa Kibongo wanachezewa makalio hovyo, wanafanya vitendo vya ngono hadharani kwa ujira wa dolari za Kimarekani mia tu.
“Kuna msanii wa Bongo muvi aliyefulia ambaye ni mke wa mtu (mcheza soka wa kimataifa) hadi sasa yupo China, nimemuona kwa macho yangu klabu akichezewa makalio kwa dola mia moja,” alisema OFM wetu.
Uchunguzi wa OFM ulibaini kwamba kuna makundi ya wanawake wa Kibongo wanaokwenda China wakijifanya wafanyabiashara lakini wengi wao hubebeshwa madawa ya kulevya ‘punda’ kisha huwa hawataki kurudi Bongo huku kukiwa na wengine wanaokwenda maalum kwa kujiuza.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment