Siku kadhaa baada ya Janjaro kuondolewa kwenye familia ya Watanashati Entertainment, Pacras Ndaki aka PNC naye amefunguliwa ‘exit door’ na kutolewa nje ya usimamizi wa kampuni hiyo.
Akizungumza na tovuti ya Times FM, boss wa kampuni hiyo, Ostaz Juma amedai kuwa hatua hiyo imetokana na utovu wa nidhamu uliooneshwa na msanii huyo kwa kutofuata sharia za Watanashati Entertainment, ikiwa ni pamoja na kufanya shows bila kuutarifu uongozi.

‘Unajua PNC alipokuja Mtanashati aliniomba nimsimamie kazi zake kwa kutumia fedha zangu, lakini unakuta anapoenda kupiga show kadhaa hanijulishi, wakati mimi ninatumia pesa nyingi sana kumgharamikia, sasa kuna umuhimu gani wa mimi kumsimamia? Ameiambia tovuti ya Times Fm.
“Sio yeye tu, na Dogo Janja, wote hawana utovu wa nidhamu kabisa, mara kumi fedha zangu nizipeleke msikitini au kwa watoto yatima nibarikiwe kuliko kukaa na watu wasiokuwa na nidhamu.” Boss wa Watanashati ameongeza.
Tovuti ya Times Fm, ilizungumza pia na PNC ambaye licha ya kukiri kuondolewa Watanashati, alikanusha madai ya Ostaz Juma ya kuwa mtovu wa nidhamu.
“Unajua mimi muziki ndio maisha yangu,nilipofika Mtanashati Ostaz Juma kanisaidia nyimbo  zangu kadhaa kurekodi studio pia alikuwa ananilipia kodi ya nyumba, sasa mwisho wa siku ikaonekana kwamba napiga show nje bila kumhusisha wakati sio kweli, yule ni binadamu kama binadamu wengine kwa hiyo mimi nasema nimefukuzwa.” PNC amefunguka.
Hata hivyo licha ya kuondolewa ghafla, mwimbaji huyo aliyewahi kufanya vizuri na wimbo wake ‘Mbona’.
“kwa sasa kazi zangu zinasimamiwa na Shebbz Entertainment ambayo pia ina studio inayojulikana kwa jina la Shebbz Record, kwa hiyo kuna project kadhaa za kwangu binafsi nimeshazifanya, kwa hiyo watu wakae tayari kwa kazi zangu mpya.” PNC ameeleza.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment