Kamati imesema mtangazaji Hadija Shaibu maarufu Dida aligeuza kipindi anachorusha redioni hapo kuwa cha ugomvi binafsi kati yake na mlalamikaji ambaye ni Karya na kwamba alichochea wasikilizaji kutuma meseji za kejeli kwa mlalamikaji jambo ambalo sio lengo la usajili wa kituo hicho. 
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji mstaafu Thomas Mihayo wakati akifafanua juu ya malalamiko ya msanii huyo akidai kipindi hicho kilimdhalilisha na kumharibia sifa kama mwanamuziki.
CIMG5204

Jaji Mihayo alisema baada ya kamati kusikiliza pande hizo mbili, inaagiza redio hiyo kumwomba radhi mlalamikaji kupitia kipindi hicho katika vipindi vitatu mfululizo kuanzia Februari 5 na maudhui ya radhi hiyo yataridhiwa na MCT. 
Alisema kituo hicho, pia kimlipe mlalamikaji Sh 500,000 kama gharama za kutayarisha malalamiko na kimuandikie barua ya kumwomba radhi ndani ya wiki moja kuanzia jana na nakala kutumwa MCT. Katika shauri hilo namba 28, 2013, Temba analalamika kushambuliwa, kukashifiwa na hata kubaguliwa na mtangazaji huyo katika kipindi chake cha Mitikisiko ya Pwani anachokirusha redioni hapo.
Vile vile Kamati hiyo imesema redio hiyo ilikiuka maadili ya utangazaji kwa kurusha kipindi kinachoshutumu watu kwa kutumia kabila lao na kilikuwa na maudhui ya udhalilishaji wa kijinsia, kinyume cha maadili na kanuni bora za uanahabari.
Source: Habari Leo
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment