Imefahamika rasmi kwamba nyimbo za waimbaji Watanzania Vanessa Mdee na Diamond Platnumz zimeingia kwenye list ya nyimbo kumi bora za Africa ndani ya chati ya radio maarufu ya The Beat 97.9.
Hii ilikua ndoto kubwa ya wasanii wa Tanzania waliokua na hamu ya kuvuka mipaka na hata kuingia kwenye headlines za taifa kubwa la Nigeria, linalomiliki sehemu kubwa ya muziki wa Afrika.
Muziki wa Wanigeria umetawala karibu kwenye kila nchi ya Afrika lakini imekua ngumu kwa muziki wa nchi nyingine kutawala kwa kiasi kikubwa namna hiyo, ndio maana hii ni good news kwa Tanzania na wasanii wake ambao mwanzoni walianza kupigwa kwenye TV chache za Nigeria ikiwemo Sound City ambapo wasanii waliopata hiyo nafasi ni Diamond na Ay pekee.
Kwenye exclusive interview na dstv.com Vanessa amesema hakuwahi kuwasiliana wala kufanya chochote na hii radio ila alishangazwa pale walipomuandika kwenye twitter kwamba wimbo wake wa Come Over umeshika namba tano.
Vanessa alikuepo nchini Nigeria mwishoni mwa mwaka jana lakini alikwenda baada ya kupata nafasi ya kuperform kwenye concert iliyoandaliwa na Radio nyingine ambapo alipata nafasi ya kukutana na wasanii mbalimbali.
Anasema: "Hii ni nafasi kubwa kwetu Watanzania, mara nyingi imekua kawaida kusikia nyimbo zao zikichezwa kwenye radio yetu ila sisi ilikua ndoto kwao lakini kazi imeanza kuwa rahisi sasa."
Msanii mwingine alietajwa kuwepo kwenye hiyo chati ni Diamond Platnumz na single yake ya Number One.
The Beat 97.9 ni Radio ambayo inajihusisha na burudani, michezo pamoja na vipindi vingine vya kijamii ambapo ipo kwenye jiji la Ibadan.

TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment