Wakati ambapo mashabiki wengi wa Ali Kiba wameendelea kumsubiria hitmaker huyo kwa muda mrefu, tumezungumza na watangazaji na madj maarufu wa Tanzania kutaka kupata mtazamo wao kuhusiana na ukimya wake. Hivi ndivyo walivyosema:

Sam Misago (Power Jams – East Africa Radio)
Hajapoteza kitu hadi sasa hivi Ali Kiba amekaa kimya tu. Ni kwamba tumezoea kusikia wasanii wanaofanya drama sana na wengine wanataka awe hivyo. Si tunamjua Ali Kiba kwenye muziki na sio mambo mengine ambayo hayahusiki. Abaki huko huko kwenye muziki, kwanini alazimishwe awe amake headlines kwa kitu ambacho hakipo? Kwasababu kama ni muziki atatoa ukiwa upo tayari anakaa kimya kwa muda anatoa wimbo. Anafanya concert anaingiza hela ananyamaza, that’s Ali Kiba tuliyemzoea maisha yote. Mi sijaona kama yupo kimya namuona ametulia, ana nyimbo zipo studio akiamua kutoa atatoa. Wakati huo ama demu mzuri, ana maisha mazuri, ana gari zuri amenunua, ila hajamuita mpiga picha yoyote aje aifanyie exclusive. Ingekuwa ni mara ya kwanza amepotea hivi, ningesema amepotea au ningesema anajishtukia. Lakini haya ndio maisha ya Ali Kiba.

Dj Majay (Xtreem Live DTV, Maisha Club)

Inategemea na plans, unajua kuna kimya ambacho kinajenga na kimya ambacho kinabomoa. Kwahiyo yeye kama amekaa kimya kwa malengo, siwezi kusema kama amepotea, lakini kama amekaa kimya ambacho hakina malengo naweza kusema amepotea. Lakini wengi wanafanya vitu kwa mahesabu kwahiyo mahesabu yake ndio yata determine kujua kama anapotea au anajijenga. Kwa mfano mimi kimya chake hicho akikaa halafu akachomoza na kitu kikali, ofcourse kinafutika ndani ya siku moja tu. Kwa mtazamo wangu mimi naona Ali Kiba bado anayo nafasi, inategemea na hesabu zake anazozifanya. Kwasababu muziki ni biashara, lazima ajue anamlenga nani na kwa muda gani. Kwahiyo akijipanga bado ana nafasi kubwa tu sababu bado ni msanii mkubwa.

Dj D-Ommy ( The Jump Off, The Switch – Times FM 100.5)

Muziki umebadilika. Ndio maana ukiangalia hata sasa hivi kuna mambo ya management. Kuna mtu ambaye muziki wake hausambazi yeye. Kwahiyo kwa Ali Kiba inawezekana akawa anajipanga kuja kwa style hiyo nyingine ili aweze kutoka maana yake sasa hivi kuna watu wengi sana wanaofanya muziki vizuri kwahiyo mpaka kupenya inabidi ujipange kweli.
Kwahiyo lazima asome soko la sasa hivi likoje. Ndio maana ukiangalia watu wa zamani wanaofanya muziki wakirudi sasa hivi wanakuwa wanafeli kwasababu hawajasoma soko la muziki la sasa hivi linataka nini na likoje. Na ndio maana tunaona kila siku watu walio on top ni wale wale. Ali Kiba ni mmoja wa wasanii mwenye kitu chake peke yake. Anaweza akaimba hata bridge au chorus lakini yale maneno ambayo ataimba Ali Kiba bado yakawa na nguvu. Kwa mfano Nai Nai watu walikuwa walikishika sana kile kisehemu cha chorus alichokuwa ameimba Ali Kiba. Kwahiyo ni mtu ambaye ana nafasi kama atajipanga na akiwa na nidhamu na muziki wa sasa hivi.

DJ Tass (Dala Dala Beat – Magic FM)

Ali Kiba anaweza akarudi, inategemea na management yake na wala sielewi mikakati yake ikoje lakini nadhani ni mtu ambaye anakuwa hayupo wazi na mambo yake na huenda akawa hajielewi yeye anataka awe nani sababu miaka inakwenda. Akishtua kitu kimoja halafu anapotea. Na Ali Kiba ni mtu ambaye hajichanganyi, hawezi kupata hata mawazo. Mtu akiwa anajichanganya na yupo karibu sana na watu labda unaweza kukuta mtu huyu anampa wazo hili mara kesho anafanikiwa. Ukikaa kimya kama yeye unaachia chance wasanii wanaokuchukulia wewe kama role model wao ambao wanafanya copy kama wewe na unakuta utamu wao unazoeleka wewe unasahaulika. Wewe nafsi inakuambia ‘wale si watoto’ hakuna cha watoto, ndio wanakua, unawaachia chance, anakua anakopi style yako mwishowe anakua Ali Kiba number 2.
Diamond hata umsearch sasa hivi kwenye mitandao yote ya kijamii yupo. Sijaona labda post za Ali Kiba. Vitu kama hivyo vinawainspire watu kuweza kufuatilia mambo yake. Akiona anafuatiliwa zaidi anazidi kuongeza juhudi zaidi. Sielewi Ali Kiba amebase wapi labda ni mtu wa kujifungua ndani. Akichukulia kwamba ‘nakaa kama nilivyozoea’ na management inayokuja ya pili labda na yenyewe itashindwa.
Millard Ayo ( Amplifaya – Clouds FM)
kiba
Mimi nimepata nafasi ya kukutana na Watanzania mbalimbali kwa mfano kama South Africa nilikuwa naenda mpaka kwenye club ambazo watanzania wapo. Dubai nilipata nafasi ya kuwauliza watu muziki gani wa Tanzania wanaupenda kiukweli Ali Kiba alitajwa zaidi. Kwahiyo inaonesha ni jinsi gani bado ana nafasi. Kuna sehemu kama Dubai, nilienda sehemu nikawa nauliza watu, bado watu wengine hawawajui akina Diamond. Kwa mfano kuna wakenya niliwauliza ‘msanii gani wa Bongo Flava unampenda’ bado wao wapo na wale wasanii kama Afande Sele, Ali Kiba. Kwahiyo bado ana nafasi, Mimi simlaumu kwa ukimya wake kwasababu wakati mwingine mtu anaweza akawa ameamua kuwa kimya kwasababu ya kujipanga kwa mambo yake na anaweza akaja na kishindo kikubwa au akaja na moto mkubwa kwenye kazi yake.
So ukimya wake unaweza ukawa sahihi wakati mwingine au unaweza usiwe sahihi. Lakini kama amekaa kimya kwasababu ya kujiandaa na kazi yake hapo inawezekana ikawa sahihi kabisa kwasababu sasa hivi kwenye bongo flava kuna competition sio kidogo. Watu sasa hivi hawako kwa msanii mmoja tu ukija na kazi nzuri watu wanahamia kwako. Wasanii ni wengi na wengi wameamua kuifanya kama ajira baada ya kuona mifano hai kwa wasanii wengine wanaofanikiwa wanajenga nyumba zao, wanaonesha mali zao, wanapata madeal makubwa kwahiyo watu wameamua kuwa serious.
Renetus Kiluvia aka Bizzo (Show Time – Next Chapter, RFA)
Binafsi mimi nadhani Ali Kiba anatambua anachokifanya kwasababu kwa level aliyokuwa amefika hakuwa tena msanii mdogo na hakuwa tena msanii wa Tanzania tu kama wasanii wengi walivyo, wanaweza wakawa wanafanya vizuri Tanzania lakini wanafahamika Tanzania tu. Ali Kiba alikuwa ameshafika mbali. Nyuma yake pia kuna jopo la watu ambao wana knowledge kubwa ya muziki na fitina za muziki pia wanazijua, fitina za muziki zipo worldwide hata Marekani pia zipo. Ali Kiba anafahamu anachokifanya na anafanya makusudi kabisa mi naamini kwasababu yeye anajijua ni mkali, analiangalia soko na anajua kabisa kuwa akirudi kesho na kesho kutwa arudi vipi. Siamini kama amepotea, siamini kama amekosa cha kufanya. Kuna nyimbo ambazo nimezikisia nyuma ya pazia, haikuwa rasmi sana, naamini kabisa akisema katika hizo bunduki adondoshe moja kiukweli kabisa kutakuwa na mtafutano mkubwa sana.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment