Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Munis a.k.a Ney wa Mitego akilishambulia jukwaa wakati wa tamasha la uzinduzi wa huduma nafuu ya Ti
go Mini Kabaang katika viwanja vya shule ya msingi Kiwanja cha Ndege Sabasaba Manispaa ya Morogoro BONVETURA KABOGO A.K.A STAMINA AKITUMBUIZA KWENYE TAMASHA LA TIGO KABAANG.
Fareed Kubanda (FID Q ) kitumbuiza mashabiki wake katika tamasha hilo.
RECHOL JOSEPHAT a.k.a Rechal alifanya vitu vyake kwenye tamsha hilo la tigo la Mini Kabaang
Hamad Ally a.k.a madee akifanya vitu vyake katika uwanja wa shule ya msingi kiwanja cha Ndege Sabasaba.
Ibrahim Mussa a.k.a Roma akionyesha uwezo katika hip pop.
Sehemu ya wananchi waliohudhuria tamasha hilo.
Msanii chipukizi wa bongo Flava Hilmali Malundo akionyesha uhidari wake wakati alipopata nafasi ya kuimba.
Wasanii wa kikundi cha salakasi cha Bowbeso kutoka jijini Dar es Salaam, Shabaan Ibrahim (Kinyonga) na Joseph Mashaka (TOOL) wakionyesha uwezo wa kucheza salakasi.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti wakati wa tamasha la uzinduzi wa huduma nafuu za mtandao wa Tigo Mini kabaang walisema kuwa endapo makampuni ya mitandao ya simu itaendelea kupunguza gharama za matumizi ya simu itasaidia kwa mwananchi wa kipato cha wastani kuongeza kipato ndani ya kaya na taifa kwa ujumla.
Augostino Andrew alisema kuwa kwa sasa mapumpuni ya mitandao ya simu yanajitahidi kupunguza matumizi ya huduma za simu lakini mtandao wa tigo ndio unaonekana kuwajali zaidi wananchi wenye kipato cha wastani hasa kupitia huduma nafuu ya Tigo Mini kabaang ambayo mteja anaweza kupata kirufushi na kupiga mitandao mingine na kuyaomba makampuni mengine nayo kuige mfano huo wa kampuni ya tigo.
“Hii huduma nafuu ya kabaang nimeipokea kwa mikono miwili, ukizingatia gharama za maisha zimekuwa juu hivyo upunguzwaji wa gharama za mawasiliano kwa kampuni hiyo umesaidia kwa kiasi kikubwa kurahisisha mawasiliano kwa mitandao yote nchini hasa kwa wananchi tuliyo na hali ngumu ya kimaisha” alisema Andrew.
Kwa upande wa Afisa Masoko wa kampuni ya Tigo Tanzania, Alex Msigala alisema kuwa kampuni ya Tigo imepunguza gharama zake kulingana na hali halisi ya maisha waliyokuwanayo wananchi wa Tanzania ili kila mwananchi aweze kumudu gharama za mawasiliano hapa nchini kupitia kifurushi cha mini kabaang kupiga simu mitandao yote.
Tamasha hilo ambalo lilifanyika katika uwanja wa Kiwanja cha Ndege Sabasaba Manispaa ya Morogoro ilipambwa na wasanii mbalimbali wa kizazi kipya hapa nchini.
Wasanii hao ni pamoja na, Fareed Kubanda “Fid Q”, Bonveture Kibogo “Stamina”, Emmanuel Munis “Ney wa Mitego”, Rechal Josephat “Rechal” na Ibrahim Mussa “Roma” ambao walitoa burudani katika tamasha hilo la Tigo Mini Kabaang.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment