
Tukio hilo lilinaswa na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Sun Ciro,Ubungo jijini Dar kulikokuwa na uzinduzi wa Shindano la Kigori wa Tanzania ambapo Jack alikuwa ameongozana na rafiki yake, jina lake halikufahamika.
Akiwa ukumbini hapo, mwanadashosti huyo aliyeonekana kula kilevi cha bei mbaya, alikuwa akiwatoa udenda wanaume kutokana na kigauni chake hicho kifupi hadi wengine kufikia hatua ya kumchana kuwa, alijichoresha kwa kutovaa ‘kufuli’.
“Huyu naye! Ndo nini sasa kutovaa kufuli kwenye kadamnasi? Wasanii wetu bwana,” alisikika kijana mmoja huku Jack akionesha kutojali.
GPL:
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment