Baby Madaha akiwa na Diamond. |
Bila kumung’unya maneno, mapema wiki hii, Baby Madaha alimvaa Diamond ambaye ni Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB) akimtuhumu kuwa na tabia za kifuska.
Baby Madaha alidai hata muziki anaoufanya Diamond kamwe hauwezi kulingana na mafanikio makubwa ya jina lake zaidi ya kubebwa na skendo tu.
CHOKOCHOKO ZILIVYOANZA
Kupitia mitandao ya kijamii, ilivuja posti ambayo ilidaiwa kutoka kwa Baby Madaha ikimpaka Diamond kuwa siyo mwanamuziki kama ilivyo kwa wasanii wengine wenye uwezo mkubwa, akitolea mfano Elias Barnaba wa THT.
Sehemu ya posti hiyo ilionesha kuwa, Diamond si msanii wa muziki bali ni mzinzi f’lani hivi anayefanya biashara ya muziki kupitia mapenzi.
“Siku wanawake maarufu nchini Tanzania watakapojitambua na kuacha kulewa penzi la Diamond, huo ndiyo utakuwa mwisho wa maisha yake kimuziki kwa sababu hatakuwa na jipya na hivyo soko lake litaporomoka,” ilisomeka posti hiyo.
UKWELI NI UPI?
Baada ya ishu hiyo kugeuka habari ya mjini na kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana, Amani lilimtafuta Baby Madaha ili kujua ukweli wa posti hiyo ndipo akatiririka aya za kuthibitisha kuwa picha haziivi, hamkubali Diamond na kudai hata kimuziki hamkubali kwani anaamini wapo wanamuziki wanaofanya vema katika gemu kuliko yeye.
“…tuseme ukweli, Diamond ni mfanyabiashara siyo mwanamuziki. Kuhusu hiyo posti iwe ni mimi nimeandika au si mimi lakini kimsingi hayo maneno yanamstahili kabisa. Mzinzi tu.
“Diamond anabebwa na media (vyombo vya habari). Kuna wanamuziki wengi wazuri sembuse yeye? Ana nini haswa?” alihoji Baby.
AMANI LAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya kusikia maelezo ya Baby kwa kifupi, Amani lilimuweka ‘pending’ kwa muda na kumwendea hewani Diamond ili liweze kujua upande wake analizungumziaje bifu hilo ambalo lilikuwa likienea mitandaoni kama moto wa kifuu.
Tofauti na matarajio ya mapaparazi wetu kwamba huenda angejibu mashambulizi makali kwa Madaha, Diamond au ‘Sukari ya Warembo’ aling’aka huku akimponda mwanadada huyo na kumshangaa:
DIAMOND AFUNGUKA
“Daaah! Huko ni kunishusha…mimi na huyo (Baby) wapi kwa wapi kamwe huwezi kunilinganisha na mtu ambaye yupo chini yangu sana, nikijibizana naye nitajishusha tu. Ingekuwa ni mtu mkubwa mwenye levo yangu hapo ningesema natakiwa kusema neno.
“Hana lolote huyo anatafuta ‘kiki’ tu kupitia mimi, nipo na dili zangu za maana nipoteze muda kwake? Atafute wa levo yake na wala si mimi.”
UZINZI VIPI?
Alipoulizwa kuhusu suala la uzinzi ambalo Baby Madaha aliumaanisha katika posti yake, Diamond aliendelea kukazia kuwa hana muda wa kupoteza kwa mtu kama Baby Madaha ambaye kimsingi ni kama ardhi na mbingu.
“Huyo anatafuta kiki tu, aachane na mimi…mbona hatufanani kabisa mimi na yeye wapi kwa wapi?” alikazia Diamond a.k.a Weka Mbali na Watoto Wazuri wa Kike.
BABY AREJEA HEWANI
Wakati mapaparazi wetu wakimalizana na Diamond, kilongalonga kimoja cha paparazi wetu kilikuwa kikionesha kinaita, ilivyokatika ya Diamond, Baby akapanda hewani kwa mara nyingine.
Safari hii alimchana laivu: “Nimeisoma upya posti yenyewe, kilichopo humu ni ukweli mtupu. Hakuna hata tone la uongo, wewe utamlinganisha Diamond na mtu kama Barnaba? Huyu ni mfanyabiashara tu, hajui kuimba kwa kutumia vyombo kama mimi.
“Diamond hawezi kupiga chombo hata kimoja cha muziki atajiitaje mwanamuziki? Anastahili kabisa ujumbe huu.”
UFUSKA
Mapaparazi wetu walilazimika kumtwanga swali Baby Madaha kuhusiana na ufuska ambao ulikuwa umetajwa katika maelezo ya awali, kama endapo Diamond ni mzinzi au yeye ndiyo mzinzi.
Katika maelezo yake, Baby Madaha aliwashangaza mapaparazi wetu kwa kutaja namna gani anaweza kumuita Diamond mzinzi. Sikia:
Amani: “Umesema Diamond si mwanamuziki, je, suala la uzinzi ni nani analo kati yako na yeye?”
Baby: “Mimi si mzinzi. Diamond ndiyo mzinzi tena sana tu.”
Amani: “Uzinzi wake upo wapi?”
Baby: “Kitendo cha kubadilisha wanawake, kufumaniwa na Wema Sepetu akiwa na Jokate Mwegelo ndiyo uzinzi wenyewe huo.”
Amani: “Kwani wewe hujawahi kuwa na wanaume tofauti? Hujawahi kufumaniwa?”
Baby: “Mimi sijawahi, yeye amewahi na hakuwahi kukanusha hivyo inadhihirisha kuwa ni kweli. Kwangu mimi kila aliyetajwa kutoka na mimi kama haikuwa kweli, nilikanusha mara moja yeye mbona hakanushi?”
Amani: “Kwani Diamond alifumaniwa na nani?”
Baby: “Acha hizo, kwani hukumbuki kipindi cha Wema? Mara alinaswa na Aunt mara na… yule ndiyo mzinzi sasa.”
KWANI WALITONGOZANA?
Kuhusu suala la kutongozwa, Baby alisema Diamond hajawahi. Cha kushangaza zaidi, alisema hata kama ikitokea siku staa huyo akamtongoza kamwe hawezi kumkubalia kwani hawaendani hata kidogo.
Alisema yeye ni mtu wa kutembea na vigogo na si vitoto kama Diamond.
“Hana hela, kamwe siwezi kumkubalia. Ni mtu ambaye ana vihela mbuzi sasa mtu kama yeye mimi wa nini? Ndiyo maana aliwahi kukimbiwa na mwanamke kwa kuwa hana hela.
“Tena yule mwanamke akaenda kwa kigogo mwenye hela, mimi na yeye ni mbalimbali kabisa. Hata muziki ninaofanya hauwezi, mimi ninaimba RnB yeye anafanya Pop, tuko tofauti kabisa,” alisema Baby pasipo kumtaja mwanamke aliyemkimbia Diamond.
TUJIKUMBUSHE PANDE ZOTE
Diamond aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na ‘totoz’ kibao wakiwemo yule wa mwanzo aliyemzingua aitwaye Sarah, Rehema Fabian, Jacqueline Wolper, Upendo Mushi ‘Pendo wa Maisha Plus’, Wema Sepetu, Natasha (Video Queen wa Wimbo wa Moyo Wangu), Najma (aliwahi kuwa mpenzi wa Mr. Blue), Jokate Mwegelo, yule demu wa Kenya na aliyekuwa mwigizaji aliyefulia ambaye ni mke wa mtu.
Kwa upande wake Baby Madaha anayekimbiza na ngoma yake ya Summer Holiday naye si haba kwani aliwahi kuripotiwa kuminya kimapenzi na yule mtoto wa mwanasiasa maarufu Bongo (jina lipo), Mwisho Mwampamba, Dokta Pakir, Juma Nature na Joe Kairuki aliye naye sasa ambaye ni mume wa mtu.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment