mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 29, niliolewa na kijana mwenye umri wa miaka 33, kwa sasa tunakaa Temeke na hatujajaliwa kupata watoto tunaishi peke yetu tu.
Mume wangu ni mwajiriwa na anafanya kazi katika Bank ya Twiga bancop, elimu yake ni chuo kikuu na mie elimu yangu ni form four. Mimi sifanyi kazi ofisini, ni mama wa nyumbani najishughulisha na vibiashara kidogo kidogo. Ila wakati tunachumbiana nilikuwa nafanya kazi kaniambia kuwa niache niende shule kwa hiyo nasubiria kuanza shule sasa ambayo naanza huu mwaka wa serikali yaani mwezi wa 7.
Swali linakuja hivi wakati tunaoana ilikuwa furaha na shangwe, tulipanga Mungu akijalia tutazaa watoto watatu. Imefikia sasa kwenye matekelezo mwenzangu mara "oh sitaki mtoto sasa hivi", hata tendo la ndoa ni sumu ndani yetu tunalala pamoja kitanda kimoja lakini ukimgusa anasema "unanitekenya usiniguse".
Mara "ohh nimechoka, ukipata mimba itakuwaje na unataka kwenda shule", nikimwambia kwani chuo wanakataza watu wenye mimba? anasema "sitaki uzae sasa", umri unakwenda, hata siku zisizokuwa za mimba hataki kufanya mapenzi. Nikimwambia kama unaogopa basi tumia condom, anasema "sitaki je ikipasuka", yaani hadi ananipa mawazo mabaya kumwazia, au ameathirika? ila tulipima kabla ya ndoa.
Nyumbani anarudi saa za kawaida na akirudi ni kitandani kutandika usingizi, je huu ni ugonjwa au nimakusudi au ni nini? nisaidieni wamama wenzangu, imefikia kipindi nikahisi labda hakuna ladha ile anayoitaka kwenye K yangu au imekuwaje jamani?
Nimeangalia hata katika simu hakuna mwanamke aliyemtumia msg au kumpigia hata akinipa simu yake siku mbili sipati msg wala simu ninayoihisi. Siku moja nikahisi labda huwa akinipa simu yake anawapa taarifa, nikaitoa kisiri kadi yake nikabaki nayo na kumpa yangu na hata hivyo ikawa vilevile sijaona simu wala msg.
Mume wangu hanywi pombe na hatumii madawa ya kulevya , ila anavuta sigara, Tokea mwaka jana mwezi wa 10 hadi leo tumefanya mapenzi mara moja tu, anadai amechoka, kila siku sijui labda nashindwa kumpa staili anayoipenda au inakuwaje, nikijaribu kumuuliza au unamwanamke nje anakataa anasema hana hamu tu.
Nikajaribu kumchunguza labda anasehemu anayo nyumba ndogo sijaona, ila chumbani kwetu kuna meza na hiyo meza kila mara naikuta inamafuta ya mgando, sijui huwa anayafanyia nini? na hata hivyo nilivyomsachi katika mifuko kuna koti la suti kalitundika ndiko anakoficha chupa ya mafuta mazito ya mgando. je anajichua nayo? atakuwa na matatizo au mimi nina matatizo? nifanyeje ili kuweza kuinusuru ndoa yangu changa?
Alivoshauri mtaalamu dinnah:
Asante sana Binti kwa kuniandikia, napenda kuchukua nafasi hii kukutaka uwe mvumilivu kutokana na majibu ya wengi ambayo ni wazi yanaweza kukufanya umtazame mumeo kivingine kabisa.
Kabla sijakupa maelezo na mbinu za kufanya, napenda kuweka wazi kidogo kuhusu jambo la mafuta mazito. Inasikitisha kuona kuwa baadhi Wabongo wanaamini kuwa mafuta mzito hutumika kwenye kufanya Ngono kusiko au Kujichua.
Ifahamike kuwa mtu huwezi kujichua kwa kutumia mafuta mazito kwa sababu hayana uterezi wa kutosha kama KY, Sabuni au mafuta ya maji (hasa baby oil) na kama ujuavyo mafuta hayo huganda ngozini badala ya kulainisha.
Hivyo basi mtu kuwa na mafuta mazito sio kithibitisho kuwa yeye ni Shoga, kuna matatizo mengi ya sirini na sehemu za kawaida ambayo yanaweza kuhusisha matumizi ya mafuta mazito.....tatizo kama Constipation (kutokupata choo), Ukavu wa ngozi, ukavu wa midomo ya nje (wanaume hawapaki lipstick au lip bum wengi hupitisha mafuta mazito kwambaali), ukavu wa viganja vya mikono, matatizo mengine ya ngozi maeneo yenye mikunjo n.k.
Unapotoa maelezo kuhusu issue ya mtu unatakiwa kusoma maelezo yake na kuyaelewa kisha una-analyse ili kutoa majibu ya kutosha ambayo yanagusa kila point aliyoigusia ambayo yeye anadhani huenda ikawa ni tatizo...........tuendelee sasa.
Wewe unajua kabisa mumeo alivyokuwa kipindi kile mnachumbiana, ni wazi kuwa ulikuwa ukifurahia tendo na hata mkawa mnapanga masuala ya kuzaa na idadi ya watoto. Kama angekuwa Shoga basi ungeligudua then na angekuwa anakukwepa na kwamwe asingelizungumzia suala la ninyi kufunga ndoa na kuzaa watoto.
Kama ilivyo kwa wanawake, wanaume pia hukumbana na mabadiliko ya miili yao kwa maana ya utendaji wao kingono, kwa bahati mbaya Mwanaume yeyote akipatwa na tatizo hili (huwapata wengi tu) hubadilika sana kutokana na hofu, mawazo na uwoga.
Mf- anawaza itakuwaje kama asipokupa watoto mliopanga, je ukijua tatizo lake utamkimbia ukaolewe na mtu mwingine? vipi kuhusu uanaume wake (Ego), je ataanzia wapi kuliweka wazi hili kwako au hata kwa Daktari n.k
Hivyo vyote vinaweza kumfanya mwanaume huyu akawa mkali na mkorofi au akawa mpole na mwenye mawazo mengi na kutumia muda mwingi kulala au kukaa peke yake hali inayoweza kuharibu hata utendaji wake kazini na pengine kupoteza kazi.
Mwanaume kama huyu anahitaji ushirikiano, kupewa matumaini, kuonyesha kuwa unamjali, unamthamini kama mwanaume na kuelewa tatizo lake. Usitegemee yeye akuambie na badala yake wewe unatakiwa kuvumbua mwenyewe, kumbuka ni mumeo na unamamlaka juu ya mwili wake sasa utumie nguzo ya Mawasiliano, busara na uanamke wako (unafundishwa kabla ya ndoa) ilikujua ukweli na hatimae kumsaidia na hatimae kupata uvumbuzi wa tatizo lake. Hilo moja.
Pili, Inaonyesha wewe ni mwanamke unaependa ku-demand kwa vile tu uliambiwa au mlipanga, kumbuka mipango siku zote hubadilika hivyo basi unatakiwa kujua namna ya kukumbushia badala yaku-demand kupata mtoto wakati mwenzakoa nahisi kutokuwa tayari au (kama nilivyosema) pengine anadhani hawezi kukuzalisha kwa vile Jogoo hawiki kama zamani na anashindwa kukuambia kwa vile anahisi aibu au kudhani kuwa utamdharau.
Tatu, umegusia kitu muhimu sana. Ilifikia mahali ukahisi huenda mumeo ameathirika na HIV na hataki kukuambukiza, lakini ukajima moyo kuwa mlipima kabla ya kufunga ndoa. Huenda ikawa kweli au inaweza ikawa sio kweli. Kama aliwahi kuonja mtu kabla ya ndoa na baadae akajaambiwa kuwa Mtu huyo anaNgoma au amefariki Dunia ni wazi atakuwa anajihisi kuwa na yeye anao na hivyo kuhofia kukuambukiza....fanyia kazi hili.
Nne, Inawezekana kabisa mumeo ana tatizo la akili liitwalo Depression ambalo kwa hapa nyumbani linaweza kuwa geni kuzungumziwa lakini lipo nalinawakumba watu wengi tu sema ni ngumu kugundua kwa mwanaume kwa vile huwa hawalalamiki unless uwe mfuatiliaji sana wa mwenendo wake.
Kutokutaka tendo la ndoa, kulala-lala, kusisitiza kwenye jambo moja, kuwa obsessed na kitu fulani mfano aina fulani ya muziki, Sigara, aina fulani ya pipi, aina fulani ya kinywaji (mf kwa case yako nitasema mafuta mazito) ni dalili chache za ugonjwa huo.
Ugonjwa huu hauponi kabisa kama ilivyo Pumu bali unatulizwa na Dawa hivyo atakuwa akitumia dawa hizo 4 life, na dawa zake kwa bahati nzuri huongeza hamu na nguvu ya kufanya mapenzi kama side effect yake ( Nina uzoefu na mtu wenye tatizo hili ndio maana nahisi linaweza likawa tatizo kwa mume pia), Mara tu akipatiwa matibabu atakuwa mume mwema na utafurahia ndoa yako....lakini je ndio tatizo? fanyia kazi hili pia......
Kutokana na maelezo yako huyu mumeo anamuamko wa hali ya juu kuhusu maendeleo yenu ya kimaisha na ndio maana anataka wewe uendelee na masomo ya juu kitu ambacho ni kizuri na unapaswa kumshukuru Mungu kwa kukupatia mwanaume mwenye kujali maisha yako ya baadae, kwani chochote kikitokea bado utakuwa na Elimu yako ambayo itakusaidia kurekebisha mambo.....sasa hebu focus on that kwanza kwa sasa.
credt to dinnah.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment