Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowasa amewataka waendesha bodaboda na watu wengine wasimwite Rais kwa sababu wanamtengenezea chuki na uhusiano mbaya na watu.
“Mbona mnataka kuniletea uchuro! Mnanitengenezea ugomvi na watu jamani…,” alisema wakati akizindua Shirikisho la Bodaboda Tanzania jana kwenye Viwanja vya Leaders, Dar es Salaam.
Lowassa amekuwa akitajwa kuwania urais katika uchaguzi ujao wa Rais na wabunge utakofanyika 2015. Hatua hiyo imekuja baada ya Lowassa kuwaeleza kuwa atafanya harambee ya kuchangisha fedha ili kila aliyeingia kwenye shirikisho la waendesha bodaboda aweze kupata pikipiki yake.
Baada ya kauli hiyo waendesha bodaboda hao walipaza sauti zao wakiimba rais,rais …..wa mwaka 2015 huku wakidai amepita hana mshindani. Aliwataka kuacha kumwita rais kwa sababu wanamtengenezea ugomvi na watu
Alisema asilimia 50 ya madereva wanaoendesha bodaboda hizo siyo pikipiki zao hivyo kutokana na hilo atafanya harambee ili kila mmoja kumiliki pikipiki yake ili waweze kujiajiri wenyewe.
“Tumeona kuna tofauti kubwa kati ya matajiri na maskini hivyo nimeona kwenye shirikisho hili asilimia 50 siyo za kwenu. Nimekusudia kuanzisha harambee ya madereva ambao hawana pikipiki ili nao wawe nazo waweze kujiajiri,” alisema Lowasa.
Waendesha bodaboda wakisukuma gari la Lowassa.
**
Waendesha bodaboda wakisukuma gari la Lowassa.
**
Lowasa aliitaka Kamati ya Shirikisho la Bodaboda kukutana naye Januari 15 mwaka 2014 ili kupanga harambee hiyo ifanyike lini na wapi.
Alisema matajiri nchini wapo wengi nitawafuata na kuwachangisha harambee wakiwemo Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi na mfanyabiashara maarufu Said Salum Bakhresa.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment