Mkali wa Sugua Gaga, Shaa ambaye sasa hivi wimbo wake  uliokaa kiswazi zaidi ndio ‘habari ya mujini’ amejibu maswali muhimu kuhusu maisha yake na muziki wake.

Shaa amefunguka wakati anaongea na tovuti ya Times FM katika mahojiano maalum kupitia segment ya Times Q &A. Times Q &A: Shaa ajibu maswali 10 muhimu, "Naweza kubadilika nikaenda kwenye gospel...ni Beyonce pekee ndiye anayenitisha kwa wasanii wa kike" (Audio)Amewataja wasanii wa kike ambao wanamtisha kwenye game, wasanii wa kiume anaowapa salute na anavyomchukulia Diamond. Mchango wa Master J kwenye muziki wake, anavyovimiss kutoka kwenye kundi la Wakilisha, mpango wake wa kuwa na familia na sifa za mwanaume anayemtaka.

Shaa amedai anaweza kubadilika na kuimba muziki wa injili, kwa nini? Fuatilia hii exclusive interview umfahamu kiundani Sara aka Shaa.

Kusimamiwa kazi zako Said Fella kumezaa matunda kwa kiasi gani?

Kusimamiwa na said Fella imeonesha kwamba ni move nzuri ambayo mimi nimeifanya. Hapo mwanzoni nilikuwa chini ya AY, na nikawa nasimamiwa na mtu fulani kutoka Kenya. Kwahiyo sasa hivi, Uswazi ndio imeniletea mafanikio ya haraka sana. Nikimaanisha kwamba Sugua Gaga imetoka tu ghafla tayari nimeshapiga show nne ndani ya mwezi, na hiyo haijawahi kutokea katika miaka yangu mitano katika muziki.

Ndio wimbo wangu wa kwanza ambao umenipatia show nyingi zaidi ndani ya muda mfupi, na ndio wimbo wangu wa kwanza uliniingizia kiasi kikubwa cha pesa ndani ya muda mfupi zaidi,  na bado nategemea…bado unajua nimeutoa mwezi wa kumi na moja  na huu ni mwezi wa kumi na mbili, na kuna mwezi wa kwanza, wa pili wa tatu bado.

Lakini kama this is the beginning, yaani mwanzo tu ndio imekuwa hivi, nategemea kwamba itaniletea mafanikio mazuri zaidi upande wa kifedha.

Kutokana na mafanikio makubwa uliyoyapata kwenye mtindo wa Uswazi, je, kuna wakati unawaza kuwa ni bora ungeanza hivi mapema? Na utaendelea na mtindo huu katika project zako?

Sijajutia nilivyoanza, mi ni mtu ambaye napenda sana kubadilika na kujaribu style mbalimbali ya muziki, muda ule nilivyoanza nilianza na style ya muziki wa crank ambao ulikuwa ni wimbo wa Zamu Yangu, nikaja nikapiga Shoga ambao ni kama kwaito na kama twist fulani hivi. Wimbo wa juzi kati hapa wa Promise, Zuku. Wimbo wa Lava Lava  Afro pop.

Kwahiyo nimekuwa nikijaribu style tofauti za muziki ingawa mi ni mwimbaji sio rapper. Kwa hiyo kwa hivi sasa nimeona sio mbaya nikijaribu style ya mchiriku, chakacha, mduara ambayo ndio mnausikiliza sasa hivi.

Na kwa sababu ni project ambayo inafanyika chini ya Mkubwa na Wanae Said Fella na Tale, kwa hiyo kuna nyimbo nyingine mbili tatu za Shaa mtazisikia upande huo. Lakini mwakani mwezi wa nane wa tisa huwezi kujua, labda ntatoka na wimbo wa gospel,labda ntarap, labda ntarudi kwenye Afro Pop huwezi kujua, huwezi kunisoma. Napenda kuwa kama Kinyonga, kubadilika na kuwapa mashabiki wangu something new, sio kila siku ugali maharage. 

Ila kwa sasa hadi mwezi wa sita ni Uswazi kwa sababu ni Project ya Mkubwa na mwanae kwa hiyo ni mchiriku mduara Shaa mtamsikia sana na hata ikiwezekana Taarab. Lakini baada ya hapo kuendelea inawezekana nikarudi kwenye style ya muziki niliyofanya mwanzoni au nikabadilika kabisa nikaenda kwenye gospel baba. Kwa hiyo ukae tu mkao wa kula ukimsikilizia Shaa.

Mkataba wako na Google kuhusu video ya wimbo wako ‘Sugua Gaga’ ukoje?

Mkataba sijasaini nao mimi kusema ukweli, mimi niko chini ya  record label ambayo ni MJ. Na MJ imemsaini Said Fella kunisimamia mimi kikazi kama manager, kwa hiyo mikataba yote inasainiwa na the record label kwa sababu wao ndio wamewekeza pesa. Katika mkataba ule ndio mimi naruhusiwa kukaa na kuupitia kuona mimi asilimia yangu ni ngapi. Lakini so far inaenda vizuri sana namshukuru Mungu. Na malipo yangu ya kwanza yanakuja mwezi wa tatu mwakani because hii ni issue ya annually sio kila mwezi, ni kila baada ya miezi mitatu hela inaingia kwenye akaunti.

Master J ana mchango gani kwenye muziki wako?

Kwenye muziki wa Shaa Master J tunamuita yeye tunamuita ni Boss Kubwa, yeye ndiye CEO wa record label yetu pale ambayo ni MJ Records ambayo mara nyingi inasimamiwa na Marco Chali. Lakini yeye ndiye CEO nikimaanisha kwamba mwisho wa siku yeye ndiye inabidi akubali project ambazo  ambazo zinafanyika, apige sahihi ndio hela itoke kutoka kwenye akaunti ya the record label. Nikimaanisha kwamba yeye ndiye anayepitisha kazi za Izzo Bizness, kazi za Quick Rocker na mimi kwa sababu ndio wasanii ambao tuko pale sasa hivi.

Kwa hiyo mchango wake ni mkubwa sana, yeye akisema hapana project haifanyiki. Angesema hapana sitaki hii kitu ya mkubwa na wanae isifanyike isingefanyika. Lakini kwa sababu yeye alipiga tick akasaini, hela zikatoka video ikafanyika, wimbo ukarekodiwa, watu wakalipwa na kitu kikatoka kwenye radio, kwenye TV.

Namshukuru sana, huo ndio mchango wake yeye na ni mchango mkubwa sana.

Wakilisha isingeweza kuwa Wakilisha bila Shaa. Unaizungumziaje kauli hii?

Mi naamini Wakilisha isingeweza kuwa Wakilisha bila mashabiki kuwakubali Wakilisha. Kwa sababu mwisho wa siku career ya msanii yoyote ni kutokana na kupokelewa na jamii. Wewe unaweza kujiita msanii lakini kama mtaani kwenu watu hawakujui na wakukubali, wewe sio msanii. Au unaweza kuwa unajua kuimba lakini wewe sio star yet, hadi jamii ikukubali na media ipige nyimbo zako.

Kwahiyo wakilisha isingeweza kuwa Wakilisha bila kukubalika na jamii.

Kitu gani ambacho unakimiss kutoka kwenye kundi la WAKILISHA?

Enzi za Wakilisha unajua tulikuwa bado wadogo, halafu mimi ndio ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuwa kwenye soko la muziki. Kwahiyo nilikuwa sijui kuandika nilikuwa naandikiwa saa zingine na Witness, saa zingine na Langa, saa zingine ilikuwa ni manager wetu ambaye alikuwa Daniel Kiondo. Nilikuwa nadirectiwa yaani, ilikuwa nikiingia ni ile ‘haya fanya hivi pita hapa’, ilikuwa rahisi sana. Tukipanda stejini tuko watatu, sio lazima mimi ndio  nipige kelele ‘changamsha audience nini’, hiyo namiss ile mbaya.

Lakini sasa hivi nikipanda stejini sasa hivi kama Shaa, uko mwenyewe macho yote kwako. Ukiingia studio kama ni wimbo ni wako wewe ndio uandike na wewe ndio uamue.

Ilikuwa inasaidia tukiwa watatu kazi zinaenda smooth, sasa hivi ukiwa mmoja inabidi uumize kichwa zaidi. Hicho ndicho nakimiss upande wa kazi.

Upande wa ushikaji, namiss kusema ukweli u-closeness wetu, urafiki wetu. Ile kwamba baada ya show au kama hakuna show tunachill tu sehemu tunapiga story, tunateta idea za nyimbo, au bwana umesikia story ya flani ‘amefanya nini’, aaah, balaaa..nini.

Kwa hiyo ule tu ushikaji nimeumiss sana. Rest in peace Langa, nimemmiss sana.

Una mpango wa kuwa na familia lini?

Mwenyezi Mungu akiwa ameipitisha, ni miaka mitatu from now.

Ni sifa gani ambazo ungependa mwanaume atakayekuwa mmeo wa ndoa awe nazo?

Kusema ukweli, kwa sababu me I’m not perfect, mimi sio malaika. Kwa hiyo ningependa kupata mtu ambaye mwenyewe..you know…sio perfect, na yeye mwenyewe anananii zake.

Unajua wanawake wengi ukiwauliza watakwambia, mimi nataka mcheshi,  awe na hela, awe na mrefu, awe ana body, awe na gari, awe na hichi…hiyo, it’s asking for too much. I’m not saying ni kitu kibaya, ni kizuri. Lakini mimi napenda mtu ambaye yeye mwenyewe yuko down to earth kwa sababu ukweli ni hakuna mtu ambaye yuko kama malaika kwamba hakosei.

Kwa hiyo mwanamme ambaye nikikaa naye nikiona kwamba huyu ni binadamu kama mimi, ana ups zake , ana downs zake, ana weakness zake na ana strength zake. Kwangu mimi naona kama huyo ndiye anafaa kuwa baba wa watoto.

Ni msanii gani wa Kike hasa wa Tanzania ambaye ukimsikiliza unaona anakutisha katika tasnia ya muziki?

Kwa wanawake msanii anayenitisha sana na natamani kuwa kama yeye ni Beyonce tu, peke yake. Tanzania ni mimi mwenyewe nikijiangalia kwenye kioo najiogopa, nasema ‘balaa dada umetiisha’.

Mi naamini kwamba, wazungu wanasema you are your own worst enemy. Kwa hiyo wewe unaposema kwamba mimi sifanikiwi..sifanikiwi, ni kwa sababu wewe mwenyewe ndio umeijiambia, kwa hiyo wewe mwenyewe ndio adui yako wewe mwenyewe, au wewe mwenyewe ndio umejizuia.

Lakini upande wa kike, niseme kwamba kwa enzi hizo wakati nasikiliza muziki wa bongo fleva, wasanii wa kike ambao nilikuwa nikiwasikia natamani kufanya muziki kutokana na wao ni Lady Jay Dee na Ray C. Especially, Ray C kwenye steji nini, nilikuwa nasema ‘eee bwana hao wadada wametisha’. Na mimi siku moja ntapanda kwenye steji na itakuwa shida. Kwahiyo hao wawili hadi kesho..si unajua hao ni malegendary.

Msanii gani wa kiume unaemkubali sana, na yupi unaesikilza zaidi nyimbo zake?

Upande wa hip hop, msanii ambaye mimi namkubali ile mbaya mbayaa ni Fid Q. Upande wangu mimi naona hata akija Jay Z, akija Nas..akija msanii yeyote toka nje akiniuliza ‘msanii wenu yupi hapa wa hip hop ambaye ni…’ aah..stop! Fid Q, apigiwe simu, njoo hapa.

Upande wa RnB napenda style ya  Barnaba, Ben Pol..yeah wako wengi. Na upande wa biashara Diamond katisha, kwa sababu amekaa kibiashara zaidi katisha sana.

Namsikiliza sana Diamond mimi kwenye radio, kwenye iPod yangu yupo, kwenye simu yangu yupo. Na mimi pia ni shabiki wake mkubwa nyimbo zake zote hajawahi kuni-disappoint.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment