Madee amefunguka kwa mara ya kwanza kuwajibu watu wanaoikosoa video ya wimbo wa Tema Tuwachape iliyofanywa na kampuni ya Ogop Videos ya nchini Kenya kwa kusema hawezi kumridhisha kila mtu.
Madee
Madee ameiambia kuwa ni vigumu kwa mtu kufanya kitu kitakachopendwa na kila binadamu.
“Mimi kabla haijatoka na haijafika kwa wananchi, tulikuwa nayo kwenye ‘cabinet’ yetu. Tumeiona, tukaruhusu itoke,kwasababu hiyo ndio video ambayo tulikuwa tunaitarajia,” amesema Madee. “Unajua huwezi kuwakataza watu kuongea,kwasababu kila mtu ana chaguo lake. Unajua ninapoimba nyimbo labda ‘Nani Kamwaga Pombe Yangu’ tayari kila mtu ana video yake anayoitaka yeye kichwani, unakuta kila mtu ana mawazo yake kichwani. Siwezi nikawafurahisha watu wote ambao wanataka video iwe hivi iwe hivi. Nilichokifanya mimi, nimefanya video ambayo tunaipenda sisi kama Tip Top Connection, ndio hiyo imetoka. Siwezi nikawafurahisha watu wote kiukweli na wala siwezi kuwachukiza watu wote. Wapo ambao wanasema wanaipenda na wapo ambao hawajaipenda. Ni kawaida huwezi kupendwa na watu wote ni dhambi na huwezi chukiwa na watu wote,” alisisitiza Madee.
Nilichokifuata mimi kule ni mabadiliko ya video zangu. Nimefanya video zangu nyingi tu Dar es salaam na kampuni za Tanzania. Nilikuwa nataka mabadiliko ya muziki wangu, kwasababu natamani kufika mbele ambako watu wengine wamefika ndio maana nikapanda ndege nikaenda Nairobi kutafuta mabadiliko. Hayo ni kati ya mabadiliko ambayo nilikuwa nayataka. Wale jamaa wana connection nzuri tu, connection yao unakuta video zao nyingi zinachezwa katika television za kimataifa, kwahiyo inakuwa rahisi na mimi kupenya kimataifa. Hayo ndio mabadiliko ambayo nilikuwa nayataka mimi. So mtu akisema kwamba video hajaipenda huwezi kuwafuraisha watu wote na wala syo suala la bei ambalo limefanya video iwe hivyo. Sisi tulienda kushoot video suala bei tumelipa kama kawaida. Mimi naona ninasonga mbele,”
Katika hatua nyingine, Madee amesema hivi karibuni anaelekea Nairobi tena kuifuata kampuni ya Ogopa kushoot video ya remix ya ‘Pombe Yangu’ ambayo amewashirikisha P-Unit.
“Unajua nyimbo tayari ishafanya vizuri East Africa nzima, hata P-Unit haikuwa kazi sana kuwashawishi kufanya hiyo ngoma. Aliyokuwa mstari wa mbele sana kutaka hiyo kitu ifanyike alikuwa ni AY. Mimi nilimpa idea AY, ‘bhana eeeh mimi nataka nifanye remix ya hii ngoma lakini sikuwa nimewapoint P-Unit, nilimtaka Prezzo kwasababu ni msanii ambaye mimi nilihisi atafit poa. Lakini AY yeye kama AY akasema ‘daah embu ngoja tuangalie’. Baada ya siku kadhaa akanipigia simu akaniambia ‘bwana P-Unit wanafanya’. AY akaorganize nao. Kwahiyo nimeanza kurecord ngoma na video naenda Nairobi, Ogopa na baada ya kumalizika itatoka,” Madee amefafanua.
“Matarajio yangu nataka kufanya vizuri East Africa mimi tayari nimeshafanya vizuri Tanzania hakuna asiyemjua Madee Tanzania. Nataka kufanya vizuri East Africa mzima ndio maana nikafanya na P-Unit ambao ni wakubwa sana. Hawa jamaa wana tuzo mbili za Channel O, kwahiyo nikikaa nao pamoja watu wasionijua watataka wanijue zaidi. Nina matumaini nitafika mbali zaidi.”
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment