MSANII Victor Peter kutoka Bongo Movie afariki dunia kwa kujinyonga katika gest moja iliyotambulika kwa jina la SAFARI JUNIOUR  ilioko maeneo ya Kisosora huko mkoani Tanga.
Hapo pichani ni mwili wa marehemu ulivyokuwa ukipakiwa katika gari kupelekwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo,
Chanzo cha habari kiliieleza kuwa msanii huyo alikuwa katika harakati zake za kushoot filamu yake mpya ambayo alicheza kama muhusika mkuu katika filamu hiyo.
Kilichowashangaza wenzake ni kwamba filamu iliisha jana Jumatatu 27/01/2014 na story ilimalizikia Vicktor kufa kwakujinyonga matokeo yake leo alfajiri Victor akakutwa amejinyonga kweli na kuiaga dunia, Mpaka sasa chanzo cha kifo chake bado hakijatambulika.

Ndugu msomaji taarifa kamili na picha za tukio zima la kuusafirisha mwili wa marehemu kuupeleka Hospitali na mengineyo fatilia hapa utayapata hivi punde
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment