Mungu ni mwema sana kwa kuwa anatupenda sote wenye wenye nacho na wasiyonacho, na anahuzunika sana na matatizo yanayojitokeza katika ndoa za leo.
Kila mmoja wetu aliye kwenye ndoa sasa natafuta cha kufanya ili aweze kumfurahisha mweza wake, iwe kitandani au hata katika mambo mengine ya kawaida.
Maana sijui nilifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Warumi 7.15 kwa hakika wengi wa wanandoa wamekuwa katika hali hii.
Baadhi hutamani sana kuwaeleza wenza wao mambo mazuri matamu, yasiyokwisha hamu ila inapofika wakati wa kusema ama kutenda ibilisi uingiza Roho ya chuki na kuleta makosa mengi ya mume ama mke ili kuondoa uzuri wake.
Na baada ya hilo, Ujikuta wakijihoji hata kwenda kwa viongozi wa kidini kutaka ufumbuzi wa haya mambo, huko upata ushauri wa aina mbalimbali.
Na wale wasiyofungamana na imani yoyote ubaki njia panda na kufikiria kuachana na mume au mke aliye naye kwa sababu ya mambo yanayojitokeza.
Nachotaka kukwambia ni kwamba Mungu aliumba ndoa katika hali ya utakatifu na hata leo bado anaweza kuimba ndoa yako, usichoke kuomba Dua usiku na mchana ukiombea uhusiano wako wewe mwanandoa na wanandoa wengine.
Kwa kuwa shetani ana njia nyingi za kuivurunga ndoa, Mungu atakupa njia ya kushinda kama utasimama kwa ajili ya kumwomba Mungu kikamilifu bila kuchoka.
Maisha ya ndoa ni mazuri yenye kila aina ya furaha yakiwa na Mungu, na majaribu ni kipimo cha imani usikate tamaa ewe mwanandoa mwezangu.
Nimeandika makala hii baada ya kupata maswahibu mbalimbali ya wanandoa, mmoja anatamani mume wake afe kwa sababu ananyanyasa kwa kuwa hana kazi ni mama wa nyumbani, mwingine mume wake ana mahusiano na wanawake wengine na sasa yuko na dada yake.
Mwingine mume wake anamtishia kumpiga kila akichelewa kurudi nyumbani, mwingine ana mnyima hela ya chakula anashinda njaa, mwingine mume wake anapenda starehe, mwingine mke wake anawanaume wengine na amemtamkia kuwa anataka kuachana naye.
Kwa maana hiyo kila mwanandoa ana kikwanzo kinacho mkwanza katika ndoa yake na ndiyo maana wanaangaika na wanaume wengine au wake wengine ila kumbuka hilo si suluhisho.
Haya yote yanatendeka ili kuichafua ndoa na kukosa utukufu, tulizana na mume wako ili uijenge familia yenye afya bora wewe pamoja na mke wako, ndoa bila UKIMWI inawezekana.
Ungana name wiki ijayo ili kupata makala zaidi za kuelimisha kuhusiana na ndoa na mahusiano kwa ujumla
CREDT NYOTA NJEMA
TUPE MAONI YAKO HAPA:
0 comments:
Post a Comment