Na imani nawe msomaji wa blog hii umzima wa afya na sasa unaendelea na majukumu yako ya ujenzi wa mahusiano yako kwa ajili ya maisha marefu yenye Amani na Upendo wa dhati. Ni ukweli usiyopingika kuwa mwanamke ni mtu mwenye upendo wa dhati ikilinganishwa na mwanaume ingawa wengi wao sasa wako kimasahi zaidi.
Mwanamke anapoamua kupenda anapenda kwa moyo wake wote na akili zake zote, na wakati wote hutumia kumfikiria Yule anayempenda.

Kwa kufanya vitu mbalimbali mfano kuwanunulia zawadi, za aina mbalimbali, wengi wao hupenda kuwanunulia nguo za ndani, viatu, saa ya ukutani, mkanda wa kiunoni wapenzi wao.


Yote hayo mwanamke anayafanya ili kuimarisha mahusiano zaidi na mpenzi wake, na kumwonyesha kuwa yeye ni wathamani ya juu zaidi kuliko mtu mwingine yoyote.


Wengi wanapofanya hivyo wanakuwa na matarajio tofauti, pengine kupokea zawadi kubwa zaidi kutoka kwa Yule anayempa zawadi, au shukrani za mara kwa mara mfano mke wangu unanifanya nionekane tofauti sana n.k.


Tofauti na hapo wengine wanaambulia patupu hivyo kukata taama ya kuendelea kumfanyia vitu vizuri, na wakati mwingine kujenga hisia za kutokuwa chaguo sahihi kwa mhusika.


Je wewe unampa mke wako zawadi au mume wako zawadi, au unaona ni utoto kupenda zawadi?


Kumbuka kila unachokifanya kina maana kubwa sana katika maisha ya mahusiano kiwe chama ama kibaya, na siku zote mahusiano yenye upendo wa dhati hayaimarishwi na mechi pekee yake.
TUPE MAONI YAKO HAPA:
LIKE PAGE YETU ILI UPATE HABARI ZAIDI

0 comments:

Post a Comment